Hii ndoto ya ajabu sana!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndoto ya ajabu sana!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magehema, Oct 27, 2009.

 1. M

  Magehema JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Nimeota ndoto ya ajabu sana, eti viongozi wa sasa/wastaafu kibao na wafanyabiashara wamejazana pale MAELEZO kila mmoja anataka kuongea na waandishi wa habari! Waliopewa nafasi ya awali kuzungumza na waandishi ni wale watuhumiwa wa ufisadi (unawajua!). Msemaji wa mafisadi kwa niaba ya wenzake wengi anakiri kwamba wao ndio wameifikisha hii nchi hapa ilipo kwa ufisadi wao, anadokeza kwamba kuanzia kwenye EPA mpaka kwenye Richmond wao ndio wahusika wakuu, baada ya kukiri, mmoja wao anasimama kwa uchungu na KUWAOMBA watanzania msamaha! [/FONT]

  [FONT=&quot]Baada ya mafisadi kumaliza na kuomba msamaha huku waandishi wakibaki vinywa wazi ikafuata zamu ya kiongozi wa jeshi la polisi, anasimama mbele ya vyombo vya habari na kukiri kwamba jeshi lake kwa wakati tofauti limewanyanyasa raia bila makosa, jeshi lake mara kwa mara limewatia ulemavu raia wasiokuwa na hatia, jeshi lake limemwaga damu za raia wema, mfano mwembechai, msitu wa pande, Zanzibar (2001) nk. Baada ya kusema hayo huku akijifuta machozi anawaomba RADHI waathirika wote na wananchi kwa ujumla! [/FONT]

  [FONT=&quot]Hii ndoto vituko, baada ya kiongozi wa polisi kumaliza, akaja yule kiongozi wa bendi yetu. Tulimpa uongozi miaka ile atuongozee bendi yetu ili iweze kushindana na bendi nyingine katika soko la muziki wa dansi.Alipopewa mic akaangua kilio kikubwa, eti anaomba msamaha, eti anasema wakati wa uongozi wake badala ya kuiendeleza bendi yetu alifikia mahali akawa anachukua magitaa, drums, mpaka keyboards anajimilikisha. Mbali ya mshahara mzuri aliokuwa anaupata na uhakika wa marupurupu kibao baada ya kustaafu, bado aliendelea kujilimbikizia vifaa vya bendi. Nae kama waliotangulia akawaomba radhi washabiki wake pamoja na uongozi wa bendi kwa ujumla![/FONT]

  [FONT=&quot]Huwezi amini ndoto imekatikia pabaya, mara nikashtuka, jasho mwili mzima ilikuwa ni saa mbili asubuhi tayari! Baadhi ya watu ambao hawakupata fursa ya kuongea mpaka ndoto yangu inakatika ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar na Mkurugenzi wa TAKUKURU. Mwenyekiti ZEC sijui angesemaje hasa kuhusu Matokeo ya uchaguzi wa 1995 na 2000? Ukiacha mwenyekiti natumaini Mkurugenzi nae angesema jambo lolote kuhusu Richmond. Hii ndoto ya ajabu sana![/FONT]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huh...! Sometimes Dreams come true!

  Mimi kwa jinsi nilivyo na mawazo MENGI, ni kwa nadra sana nikaota ndoto ndefu namna hii!

  Mungu akujaalie safari ingine uote ndoto ya PESA!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  teh teh teh
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mkuu ndoto yako hii inapaswa wahadithiwe watanzani wengi zaidi, tafadhari itume kwenye magazeti watanzania waisikie na imani ni ndoto ya TZ wengi, hihihihi isingekuwa si hutu tuaibu twangu ningeifanyia plagiarism hii kitu imesimama.
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Siku zote wanaharakati huwa na mawazo juu ya chao,sasa haya mawazo hayawaachi peke yao hata dakika moja,ndio maana huota ndoto zenye mtazamo wa harakati kama hizi,lakini wazinzi zao ni zile za kuchafua shuka tuu,Asante sana nimeipenda hii!!
   
 6. M

  Magehema JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimependa kicheko!!!!
   
 7. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hii inaonyesha kiasi gani umeguswa na hujuma zinazofanywa hapa nchini, big up!!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Siku nyingine uwe makini kama umelala na my wife wako unaweza ukampa ndoo au unampa bonge la kabari kwa hasira ukifikiri ndo mkuu wa Mafisadi. hahahahaa!

  sio utani, itume hii kitu kwenye magazeti watu wengi zaidi waisome.
   
 9. GP

  GP JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  na wewe nenda pale MAELEZO kahadithie hiyo ndoto kwa waandishi wa habari.
   
 10. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mbona sijakuelewa? Naenda kupumzika kidogo, nikirudi simulia tena
   
 11. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Kaka ni kweli lakini huyu jamaa mbona ndoto imeenda kimpangilio sana!! Mimi huwa naweza kuota labda niko shamba nalima, mpaka ndoto iishe nakua niko Dar ofisini. ila kaka kama ndoto kweli natamani leo uote tena angalau ifike mwisho aisee. Jombaa imekaa sawa
   
 12. M

  Magehema JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Tnx Mkuu, natumai watu wa media tunao humu, they are free to download/copy n paste and share it with more wapiganaji! Ila haijaisha ndoto yenyewe!
   
Loading...