IRINGA ONE
Senior Member
- Mar 19, 2015
- 139
- 96
Habari Jf , Naomba Niende Moja Kwa Moja Kwenye Mada, Mimi Ni Mwanaume Wa Miaka 36 Ambaye Nimesoma Mpaka Ngazi Ya Kati, Historia Ya Elimu Ni Kuwa Kidato Cha 2 Hadi 4 Nilikosa Ada Hivyo Kupata Adha Nyingi Sana, Ikiwemo Kurudishwa Nyumbani Na Kupigwa Viboko Kwa Miaka Yote Hiyo Pale Ninapoenda Nyumbani Na Kurudi Bila Ada! Tatizo Ni Hili, Baada Ya Kupata Ajira Mkoa Fulani Nimekuwa Nikiota Nipo Shule Nafukuzwa Kuwa Sijalipa Ada Na Adha Nyingine, Ambapo Baada Ya Kutoka Ndotoni Huwa Na Mfadhaiko Sanaaa Na Mapigo Ya Moyo Kuwa Juu. NB. KUMBUKA DENI LA SHULE NILISHALIPA WAKATI NACHUKUA VYETI HIVYO SIDAIWI. Wandugu naja kwenu kwa utabiri wa ndoto hii, AHSANTENI.