LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 455
- 1,665
Naombeni mnitafsirie hii ndoto,
Najua tunaotaga ndoto nyingi ila kuna ndoto ukiota inakuwa ngumu kuisahau
Ilikuwa hivi:
Sikumbuki tulikuwa wangapi ila ilikuwa ni zaidi ya watu watatu, tukiwa tunatembea pembezoni mwa reli mara likaja treni la mizigo likawa limepooza mwendo, tukaomba lifti tukapanda mimi nikawa nimekaa na dereva.
Sasa kufika kwa mbele tukakuta hakuna reli yaani ikawa tu njia ya kawaida ya vumbi nikamuuliza dereva akaniambia nichukue nimsaidie kuendesha.
Kweli nikawa naendesha japo njia ilikuwa mbovu sana makorongo na magogo mengi ila nilijitahidi sana kuipitisha treni katika njia nzuri hata kuipitisha mashambani nikikuta njia mbovu sana lakini kulikuwa na uhakika wa 100% mia kwamba huko mbele tutaingia kwenye reli.
Naombeni tafsiri ya hii ndoto.
MSHANA JR nakusubiria hapa.