Hii ndoto ameota mchumba wangu

Hii ndoto ameota mchumba wangu

mwalidebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2016
Posts
426
Reaction score
251
Usiku wa saa 6 kuna jambo lilinitokea la ajabu sana, nikiwa nimemaliza kuomba nikalala lakini sikuwa na usingizi nikahisi kama kuna mtu amesimama kitandani ghafla nikahisi uzito wa mwili na macho nikajitahidi kukemea ghafla nikaona kivuli cha Mwanamke na mkono wake ukishika tumbo langu nikajitahidi kukemea na kutaka kuinuka nikaweza kuinuka

Mara nikasikia tumbo likiunguruma nikakaa kitandani na kuanza kuomba hadi saa 6 na dakika 45 nikalala, kwenye saa 7 na dakika zake nikapitiwa usingizi nikaota niko mazingira ya chuo mimi na wenzangu ambao nilimaliza nao secondary akiwemo Philbeth Jacqreen pamoja na Arafa tukiwa darasani tukaona wenzetu wakicheza kwaya

Na wengine wakifanya biashara ya nguo lakini tukiwa humo darasani tukashauriana kwa sababu ya kelele tuweze kutoka na kwenda kusimama nje tukiwa tumebeba mabegi yetu tukaelekea upande wa madarasa mengine ambako kuna walinzi na hawaruhusu kuingia ila nikawaona hao mabinti watato niliokuwa nao wakiingia

Lakini hawakutoka na kufungiwa mlango ndani mabeg yao yakatupwa nje sasa mimi nikasema mbona umewafungia mlango akasema yule kijana mlinzi yakuwa huku haruhusiwi kupita mtu wala kuingia ni sehmu ya Jeshi kwa hiyo hawa hawawezi kutoka tena

Basi pembeni ya ule mlango kulikuwa na viti na mabenchi kama ya Zahanati nikaweka begi langu nikasema niende Kuwaangalia wale wanafunzi wenzangu darasani ambao tuliwaacha wakicheza kwaya lakini cha kushangaza sikuwakuta na niliwakuta wanafunzi wengne na mimi nikarudi kuchukua begi langu

Ndipo nilipowakuta vijana wengne kama wanne hivi pale nilipoacha begi langu sukuliona nikajaribu kutafta nikalipata hilo begi pembeni kwa nje limetupwa lakini nikaamka kutoka usingizini baadae nikaota tena nipo hayo maeneo ya chuo ambapo niliacha begi nikaanza kulitafta sikuliona wale vijana wakiwa wamekaa paleple wakaniambia katafute kule Porini

Nikaenda ambako kumefyekwa nikakuta mabegi mengi yametupwa mengine mapya na mengne machakavu nikawa natafuta bila mafanikio. Nikiwa nalia nikafanikiwa kuliona begi rangi ya kijeshi likiwa jipya nalo miongoni mwa yale yaliyotupwa nikajisemea akilini mwang bora nichukue begi hilo kuliko kurudi nyumbanu bila begi

Nikiwa bado natafuta la kwang bila mafanikio nikaamua kuondoka na ndipo niliposhtuka kutoka usingizini na kuitafakari hiyo ndoto ikiwa na maana gani kujirudia mara mbili nikiwa natafuta begi!

Unaweza nisaidia tafsiri hiyo ndoto mtumishi

received_2272229882822206.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kuandika sentensi nzima unaona uvivu ama? Anyway ndoto yenye maana ni moja tu ile ambayo ukiota unafungua mlango wa chooni ni mtego huo shtuka kabla hujaachia zigo kwa kitanda. Zingine porojo tu.
 
Mchawi alifika kwako ukiwa umelala na kwa bahati nzuri ulikuwa umesali kabla ya kulala kwani sala ilikuwekea ulinzi. Wachawi huzinguka kila mahali kufanya kazi waliyotumwa ya kuiba na kuharibu na kuua. Dawa yao ni maombi makali.

Lakini uliota ndoto, kwani mchawi aliingia katika ulimwengu wa roho na kuanza kucheza na roho yako ukiwa umelala. Alichokuwa anafanya ni kuwanga au ‘kuprogram’ roho yako kupitia ndoto ili akuibie mafanikio.

Ukiota mazingira ya shule manake unarudishwa nyuma katika maisha yako. Hilo ndilo lengo la yule mchawi. Unapaswa kusali kwa nguvu zaidi na kuelekeza mashambulizi kwa mchawi huyo kila siku kuzuia kazi za kichawi kwenye maisha yako.

Rudisha yale yaliyoibwa kichawi kutoka kwako kwa njia ya maombi ya nguvu. Asubuhi na jioni kabla ya kulala hakikisha unasali na kujiweka mikononi mwa Mungu na utaepuka balaa nyingi sana.
 
Mchawi alifika kwako ukiwa umelala na kwa bahati nzuri ulikuwa umesali kabla ya kulala kwani sala ilikuwekea ulinzi. Wachawi huzinguka kila mahali kufanya kazi waliyotumwa ya kuiba na kuharibu na kuua. Dawa yao ni maombi makali.

Lakini uliota ndoto, kwani mchawi aliingia katika ulimwengu wa roho na kuanza kucheza na roho yako ukiwa umelala. Alichokuwa anafanya ni kuwanga au ‘kuprogram’ roho yako kupitia ndoto ili akuibie mafanikio.

Ukiota mazingira ya shule manake unarudishwa nyuma katika maisha yako. Hilo ndilo lengo la yule mchawi. Unapaswa kusali kwa nguvu zaidi na kuelekeza mashambulizi kwa mchawi huyo kila siku kuzuia kazi za kichawi kwenye maisha yako.

Rudisha yale yaliyoibwa kichawi kutoka kwako kwa njia ya maombi ya nguvu. Asubuhi na jioni kabla ya kulala hakikisha unasali na kujiweka mikononi mwa Mungu.
Sina jinsi au namna nzuri ya kushukuru ila naomba upokee hii shukurani yangu Asante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uck wa saa 6 kunajamb lilinitokea la ajabu san, nikiwa nimemaliza kuomba nikalala lakn sikuwa na ucngz nikahc kama kunamtu amesmama kitandan ghafla nikahz uzto wa mwili na macho nikajitahd kukemea ghafla nikaona kivul cha mwanamke na mkono wake ukishka tumbo langu nikajitahd kukemea na ktaka kuinuka nikawez kuinuka mara nikackia tumbo likiunguruma nikakaa kitandan na kuanza kuomb had xaa 6 na dakika 45 nikalala, kweny saa 7 na dakka zake nikaptiwa ucngz nikaota niko mazngra ya chuo mim na wenzang ambao nilimaliza nao secondary akiwemo philbeth jacqreen pamoja na arafa tukiwa darasan tukaona wenzet wakicheza kwaya
Na wengine wakifanya biashara ya nguo lakn tukiwa hm darasan tukashaurian coz ya makelele tuweze kutoka na kwenda kusma nje tukiwa tumebeba mabeg yetu tukaelekea upand wa madaras mengne ambako kunawalinz na hawaruhs kuingia ila nikawaona hao mabint watat niliokuwa nao wakiingia lakn hawaktoka na kufungiwa mlango ndan mabeg yao yakatupwa nje xaxa mim nikasema mbna umewafungia mlang akasema yule kijana mlinz yakuwa huk haruhsiw kupta mtu wala kuingia ni sehmu ya jesh kwa hy hawa hawawez kutoka tena bhc pemben ya ule mlang kulikuwa na vit na mabench kama ya dhahanat nikaweka beg lang nikasema niende Kuwaangalia wale wanafunz wenzang darasan ambao tuliwaacha wakicheza kwaya lakn cha kushangaz ckuwakta na niliwakta wanafnz wengne na mim nikarud kuchukua beg lang na ndipo nilipowakta vijana wengne kama wa4 iv pale nilipoacha beg langu ckuliona nikajarb kutafta nikalipat hlo beg pemben kwa nje limetupwa bt nikaamka kutoka ucngzn baadae nikaota tena nipo hay maeneo ya chuo ambpo niliacha beg nikaanza kulitafta ckuliona wale vijan wakiwa wamekaa paleple wakaniambia katafte kule polin nikaenda ambako kumefyekwa nikakta mabeg meng yametupwa mengne mapya na mengne machakav nikawa natafta bila mafanikio Nikiwa nalia nikafanikiwa kuliona beg rang ya kijesh likiwa jipya nalo miongn mwa yale yaliyotupwa nikajisemea akiln mwang bora nichukue beg hl kuliko kurud nyumbn bila beg nikiwa bd natafta lakwang bila mafanikio nikaamua kuondoka na ndipo niliposhtuka kutoka ucngzn na kuitafakar hy ndot ikiwa na maana gan kujirudia mara mbili nikiwa natafta beg! Unaweza nisaidia tafsr ya hy ndoto mtumishView attachment 1021077

Sent using Jamii Forums mobile app
Picha ni ww
 
Hakuna mwanadamu anayeweza kukutafsiria ndoto

Mungu pekee ndiye hutoa tafsiri

Hivyo kuna vipengele kadhaa unapaswa kuvifuata unapotoka ndotoni na hupata tafsiri hapo

Kamwone mchungaji/shehe wako atakupatia haya maarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kama mchumba wako anakusumbua umtafsirie ndoto za kawaida kama hizi na unakubali hadi kuhangaika huku JF, basi tafsiri yake ni kwamba hiyo ndoa yenu haitadumu, atakuboa baada ya muda mfupi sana na usumbufu usio wa lazima!
 
Nimegundua Uku JF wengine ni vichaa na nusu.... Huyu anahitaji tafasiri kweli ya ndoto yake,Sasa Kuna vichwa boga watamdiscarrage, wengi wanauthi Hadi bhasi.

90% ya ndoto zinamaana kwenye maisha ya muotaji.

Pia ni kweli sii kila ndoto yafaa kupata maana kirahisi... According to mchungaji wangu Mastahi, Alinifundisha .. ndoto yoyote unayoona imekuja nzuri,, ibariki na kuipa ulinzi was roho mtakatifu, na Kama imekuja ndoto mbaya unaona kabisa sii nzuri kwako,hata Kama uelewi.. muombe Mungu akuepushe na baya lolote lililopo nyuma ya ndoto ile... Kwa ufupi naweza sema hivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom