Hii ndoa ime swihi kweli?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
Wiki iliyopita nilialikwa kwenye harusi ya rafiki yangu. Ameolelwa na mzungu na ilibidi Sheikh aitwe mzungu amkane Yesu kwanza.

Tulipika pilau chai ya viungo, maandazi, vitumbua visheti. Bwana harusi kumbe alikiandaa na sanduku 5 za bia, box 2 za wine na chupa 5 za Jack Daniel. Mkewe kwa mstuko alimwambia pombe hairuhusiwi. Bwana yule alisema iwekwe jikoni lakini walevi wanywee kwenye vikombe vya chai Sheikh asione.

Hakumfahamisha ndugu yake yeyote, bwana harusi alikuwa mwenyewe lakini wapambe wa bibiharusi tulitinga na madera.

ilimchukua mwaka mmoja kutafakari kwakua shost alimwambia hawezi kuishi bila ndoa.
 
Kwahiyo mzungu alikuwa Mkristo anamuoa binti wa kiislamu. Mzungu kasilimishwa na shehe kwa kumkana Yesu (ndo kusilimishwa? au Sio?). Baada ya hapo huyo mzungu kaandaa vilevi lakini bibi harusi (mwislamu mwenye itikadi Kali) hakupenda. Mzungu katoa wazo wanywee vilevi kwenye vikombe kama chai ili shehe asijue?? Ebu tufafanulie.....!
 
Kwani pombe ziligidwa msikitini au ukumbini..?

Nimegundua kumbe hata Kiswahili sijui vizuri.
 
Ndivyo ilivyokua
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…