Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,604
Frank Pasua kichwa
Ommy mfanya biashara
Chomba kauza simu jana chini ya Mnara
Wale wanaonibip najua hawana dola,
Hawawezi kupiga muda mrefu kama Babra,
Anayeweza lea simu anaeweza familia,
Dola kumi kwa wiki wee mwenyewe fikiria,
Simu uwe na dili simu sio ubishororo,
Simu ina wiki mbili haijaita huu mgogoro,
Ubitozi haufai ya nini unabeba toi,
Ili masista duu wasijue we mlalahoi,
Wale kina Chomba naomba tuwe makini,
Mwenzio nishaziacha simu nyingi tu mezani,
Na ukipata demu pia akili kichwani,
We unapiga bao mwenzio mkono mfukoni.
Yaa kama unaongea na simu, bora upaki iyo gari,
Na kama we unabisha jua ni mbele ajali,
Ongea kwa dirishani vibaka uwape zari,
Piga yangu mkononi lete dili acha stori,
Watu bize na meseji yaani kila kukicha
Yaani mjini usiseme wanavyogongana vichwa,
Ukiuliza aina gani ni siemens ama nokia,
Yaani mambo ya gemu na picha yamenivutia,
Simu yangu ofisi, simu yangu ibilisi,
...
Natamani jamaa aje na version mpya ya Simu yangu, hasa wakati huu wa ma-smartphone.