Bundewe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 400
- 141
Mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.
Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya msingi pekee lakini nao wamechukua fomu, kuna ambao wamejiuzulu kwa kashfa za wizi nao wamechukua fomu.
Maoni yangu ni kwamba peformance ya kiwango cha chini iliyooneshwa na rais aliyepo sasa imesababisha hali hii.
Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na CCM kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark Mwandosya,
2. Mwigulu Nchemba na
3. John Magufuli,
Na huenda John Magufuli akawabwaga wenzie katika hatua hiyo na kupewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM. Mpambano kati ya Dr. Magufuli na Dr. Slaa utakua na msisimko wa aina yake.
Tupia maoni yako, unadhani ni nani wana nafasi ya kupitishwa na CCM?