Hii ndiyo TBC halisi

Hii ndiyo TBC halisi

SUPER PREDATOR

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
2,093
Reaction score
725
TBC ya Leo ni ile inayoonyesha upendo na mambo mazuri tu. Kwa mfano kama wanaonyesha kipindi cha wanyama basi utaona nyumbu wanakula majani bila bughuza yoyote na pembeni utaona simba wamepumzika, na simba wengine wanawabeba watoto wao kwa upole kwenye midomo yao.

Harafu utasikia mtangazaji wa tbc anasema nyumbu ni wanyama wapole sana na wenye ushirikiano wa hali ya juu sana, hawagombani wala kufokeana. Baada ya hapo wanaamia kwa simba utasikia simba ni mnyama mpole sana na hasa kama ameshiba, tena huwabeba watoto wao kwa upole sana.

ITV ipo vile vile wao utaona nyumbu anavyohangaika kutafuta malisho na maji, nyumbu wanavyopigana, nyumbu wanavyokufa kwenye mazingira tofauti. Harafu utamuona simba anavyowinda, anavyokula, anavyoua simba watoto na wanavyouana wao kwa wao.

Harafu utamsikia mtangazaji anakwambia nyumbu hula kwa tahadhali sana kwa sababu anajua muda wowote atakamatwa na kuliwa na wanyama wanaokula nyama, utamsikia mtangazaji anakwambia simba anapowinda huwa hana huruma mpaka apate chakula chake na kushiba na wakati wa kula simba huwa hawana ushirikiano Mara nyingi utakuta wanagombana wakati wa kula.

Sasa kutokana na utangazaji wa aina hiyo watoto wengi wanapenda kuangalia TBC, na kutokana na utangazaji huo watu wazima wengi wanapenda kuangalia ITV hivi ni kwa nini?.
 
Kwako SUPER PREDATOR mwandishi wa hii tamthilia ya Nyumbu na Simba, ni mhusika yupi kati ya hao TBC na ITV amehegemea katika maisha halisi ya hao wanyama?
 
Last edited by a moderator:
ITV; Mgawo wa Umeme umeathiri shughuli nyingi na kusababisha mdororo wa uchumi na hali ya upatikanaji wa Umeme bado ni tete.
TBC; Serikali bado inashughulikia kwa makini upungufu uliojitokeza wa Umeme kwa maeneo kadhaa na kuahidi hali itatengemaa ndani ya muda mfupi.
 
ITV; Mgawo wa Umeme umeathiri shughuli nyingi na kusababisha mdororo wa uchumi na hali ya upatikanaji wa Umeme bado ni tete.
TBC; Serikali bado inashughulikia kwa makini upungufu uliojitokeza wa Umeme kwa maeneo kadhaa na kuahidi hali itatengemaa ndani ya muda mfupi.

Hahahahaaa mweee wewe chakaza unataka kunigombanisha na serikali
 
Nahisi hili fumbo litakua juu ya akili za wengi kuling'amua,inahitaj great thinking na hapo ndipo maana ya Jf inapodhihirika,asante mleta uzi!
 
Back
Top Bottom