sijui nitasema vibaya lakini huu ndio ukweli
- tunapenda unyonge na hali ya kuonewa huruma kila mahala na unyonge wetu tunaukumbatia kama silaha kwetu tukiamini kuwa haya ni maisha.
- kipi bora awe na kitambulisho atakacholipia shilingi 20,000 kwa mwaka ambacho kitamwezesha kuwa na fursa zifuatazo
- kuwa na uhakika wa kuuza bidhaa zake kwa kadri ya matamshi ya selikali
- pili kupunguza gharama za uendeshaji ambazo alikuwa kwa siku anatozwa si chini ya shilingi 500/- sawa na 15,000 na shilingi 180,000/- kwa mwaka.
- wengi hamjui vizuri changamoto zilizopunguza vitambulisho hivi kwa kuwa wengi wenu hamjawahi kufanya kazi na watu hawa mkaona wanavyonyanyaswa na huu ni mwanzo zipo fursa nyingine ambazo zinaweza kutazamwa siku zijazo ikiwa ni kuangalia jinsi ya wao wanawezaje kuwa na bima ya afya kwa unafuu na pia kujiwekea akiba ya uzeeni katika mifuko ya jamii achilia mbali mazingira ya wao kuanza kuaminiwa na taasisi za kifedha siku zijazo
- hivyo sio kila kitu cha kubeza