Hii ndiyo sababu ya CCM kuwa na watia nia wengi kwenye Ubunge

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Wengi wanatafuta kujulikana na kutambuliwa na mamlaka ya uteuzi ili wapewe vyeo vya DC, DAS, RC, DED etc

Hiyo ndiyo njia pekee ya kufahamika ndani ya chama, hivyo wanachama wote wenye elimu zao wanaofikiri wanafit kwenye vyeo tajwa hapo juu wanatia nia
 
Mods unganisha na hii picha
IMG_20200712_125235.jpeg
 
Wengi wanatafuta kujulikana na kutambuliwa na mamlaka ya uteuzi ili wapewe vyeo vya DC, DAS, RC, DED etc.

Hiyo ndiyo njia pekee ya kufahamika ndani ya chama, hivyo wanachama wote wenye elimu zao wanaofikiri wanafit kwenye vyeo tajwa hapo juu wanatia nia.
Upo sahihi ni sababu ya mfumo mbovu na katiba mbovu tuliyonayo kumpa uMUNGU mtu mmoja, iliakufahamu lazima uingie huko hata kama hupataki
 
Wimbi la watu na vijana wanaotia nia wengi wao wanajenga CV tu kwa baadaye ila lazima wajue misingi na taratibu za hadi mtu anapigiwa kura na wajumbe wale wa mashinani. Yaani wale wajumbe wa chini kabisa huku inabidi uwa-win hawa kwanza, sasa hiyo ku-win sasa...

Mimi juzi nilikua shamba huko Bagamoyo nikawa naongea na vijana wangu ambao ni wakereketwa wa chama wale kindakindaki wanasema wao wanawaangalia tuu na fujo zao wanasemaa hiiii.

Ubunge watapita wazoefu tuu trust me. Hawa kina tivu ake na the likes wanajitekenya na kucheka wenyewe tu.

Uzi tayari
 
Mkuu ku wa win hao wachini ambao wengi ni masikini wa kutupwa inahitaji uwe na angalau 50-100M,asiee mie nilijaribu nikaona natwanga maji kwenye kinu.yaani hao watu wa chini wenyewe hawataki kusikia mambo ya sera wala nini wenyewe wanataka mpunga.
 
Hivi kutia nia napo kunaongezwa kwenye cv... Huu ni uzezeta tu... Labda ukishateuliwa kuwa mgombea kamili kidogo inaleta maana napia jimbo gani ama kata gani...
 
Kiinua mgongo cha 250m baada ya miaka mitano kinashawishi. Vijana wamechoka kuambiwa wajiajiri huku wanaosema hivyo hawatoki mjengoni na kuonesha mfano.
 
By Dotto Bulendu
Leo asubuhi nimeamka na ujumbe kutoka Kwa rafiki yangu wa kitambo tulisoma nae sekondari ngazi ya O-Level juu ya Yeye kutia nia ya kugombea Ubunge,Mazungumzo yakawa Hivi...

Rafiki:Chief salama?upo Mwanza?

Mimi:Salama chief,hapana,nipo Dodoma,vipi mkuu asubuhi sana?

Rafiki;,Nakutaarifu leo naenda kuchukua fomu ya kuwania ubunge,Wewe vipi huna mpango?

Mimi;Oooh hongera sana Chama gani?mimi binafsi sijawahi Kuwa Na ndoto za kuingia Kwenye siasa.

Rafiki;Ooooh,poa,nagombea kupitia tawala,CCM

Mimi;,Hongera chief,lakini mboka Huko uliondoka kitambo,wapiga Kura wanakukumbuka kweli?

Rafiki;,Oooh,unadhani tunachukua fomu ili tupitishwe,sisi tunasaka nafasi tu ya CV zetu kupita mbele ya uso wa mwenyekiti,siunajua unaweza Kuta Una CV nzuri Ila Mzee hakufahamu,Sasa CV zetu zimeshiba unaweza jikuta unapata kauteuzi.

Mimi;,Hahahaaaaaa,Kumbe Hii ya kila mtu kutaka kugombea ni mkakati wa kuhakikisha angalau CV inakufikia Mzee?

Rafiki;Ndiyo Maana yake,Wewe siunaona wasomi wote wameenda kuchukua fomu hata Kama jimboni hujulikani,Haya maisha wacha tukapambane,Maana tumesoma halafu hatuna pesa.

Mimi;,Sawa Bwana ,kila jema.
 
Ni kweli mkuu ,wengi waliovuka na kuingia kwenye top 3(2015) wameteuliwa kuwa DED,DAS,RAS,DAS,RC,DC etc Kwahiyo ni njia nzuri ya kulikuza jina mbele ya JIWE.
 
By Dotto Bulendu
Leo asubuhi nimeamka na ujumbe kutoka Kwa rafiki yangu wa kitambo tulisoma nae sekondari ngazi ya O-Level juu ya Yeye kutia nia ya kugombea Ubunge,Mazungumzo yakawa Hivi...

Rafiki:Chief salama?upo Mwanza?

Mimi:Salama chief,hapana,nipo Dodoma,vipi mkuu asubuhi sana?

Rafiki;,Nakutaarifu leo naenda kuchukua fomu ya kuwania ubunge,Wewe vipi huna mpango?

Mimi;Oooh hongera sana Chama gani?mimi binafsi sijawahi Kuwa Na ndoto za kuingia Kwenye siasa.

Rafiki;Ooooh,poa,nagombea kupitia tawala,CCM

Mimi;,Hongera chief,lakini mboka Huko uliondoka kitambo,wapiga Kura wanakukumbuka kweli?

Rafiki;,Oooh,unadhani tunachukua fomu ili tupitishwe,sisi tunasaka nafasi tu ya CV zetu kupita mbele ya uso wa mwenyekiti,siunajua unaweza Kuta Una CV nzuri Ila Mzee hakufahamu,Sasa CV zetu zimeshiba unaweza jikuta unapata kauteuzi.

Mimi;,Hahahaaaaaa,Kumbe Hii ya kila mtu kutaka kugombea ni mkakati wa kuhakikisha angalau CV inakufikia Mzee?

Rafiki;Ndiyo Maana yake,Wewe siunaona wasomi wote wameenda kuchukua fomu hata Kama jimboni hujulikani,Haya maisha wacha tukapambane,Maana tumesoma halafu hatuna pesa.

Mimi;,Sawa Bwana ,kila jema.

Nimeanza kuelewa 🤔
 
Nimeona ccm vijana wengi sana wanamiminika kuchukua fomu kuwania ubunge na udiwani. Nini maoni yako?
 
Natumaini ni wazima wakuu,Nawasalimu kwa heshima zote.
Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa wale wote waliotia nia kwa sababu ni haki yao kikatiba,kupiga kura hata kugombea pia. Na hata sasa ambao hatujatia nia naona bado tunajitasimini tuone kama tunaweza kutia nia 2025.

Katika pitapita zangu na kufatilia watia nia kadhaa hasa wale ambao ninawafahamu,nimepata kupenyezewa info kidogo,nikaona eh kumbe mambo yapo hivi mpaka nikajiuliza mimi nimekwama wapi.

Watu wengi wanajiuliza mpaka flani katia nia kumbe ubunge ni rahisi kiasi hiki? Rafiki yangu kumbe sisi tunafikiria ndani ya boksi kuna watu wamewaza mbali sana na wana malengo zaidi ya hayo ya kuchaguliwa kuwa wabunge.

Unaambiwa watu wana lengo la CV zao kupita katika uso wa mwenyekiti,na wala sio huo ubunge,watu wanajua pale kwenye ubunge sipati ila CV yangu ilivyoshiba ikipita kwenye uso wa mwenyekiti hata ukatibu tawala siwezi kukosa.

Hapa ndio unakuta vijana wengi,watu tofauti hata wale ambao tuliona hawawezi kutia nia nao wamejitokeza lengo ni CV zipite kwenye uso wa mwenyekiti.

Nawasilisha.
 
Mleta mada huo ndo ukweli!
Mwaka 2015, Jiwe aliteua mskada kuwa wakurugenzi huko mawilayani na mikoani kwa hiyo watu wanadhani zali litaibuka tena!
 
Back
Top Bottom