Hii Ndiyo Maana Ya 'Black History Month'.

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Ni mwezi maalum kwa ajili ya kukumbuka watu na matukio muhimu katika historia ya mtu mweusi. Sherehe hizi husheherekewa nchini Amerika, Canada kwenye mwezi wa Februari, na nchini Uingereza au United Kingdom na Netherlands husheherekewa kwenye mwezi wa Oktoba.

Sherehe hizi zilianzishwa nchini Amerika mwaka 1926, ambapo mwanahistoria Carter G. Woodson and the Association for the Study of Negro Life and History walipotangaza wiki ya pili ya mwezi Februari kuwa wiki wa Negro au 'Negro Week'. Wiki hii iliteuliwa kwa sababu ni kipindi ambacho Abraham Lincoln alizaliwa yaani tarehe 12-Februari, na Fredrick Douglass aliyezaliwa tarehe 14-Februari.

Tuungane pamoja kusheherekea kipindi hiki muhimu, lakini wakati tukisheherekea, inatulazimu kutenda yale yaliyohubiriwa na wale waliosafisha njia kwa ajili yetu.

Kumbuka:....'mtu bila uelewa wa historia yake, asili yake na utamaduni wake, ni sawa na mti bila mizizi'--Marcus Garvey.

Kipindi hiki (Black History Month) kisitafsiriwe vibaya na kuonekana kama 'black supremacy', la hasha. Ni tukio kama yalivyo matukio mengine muhimu ambayo watu fulani huyaheshimu.

*Je, kwa kipindi hiki unamkmbuka mtu gani mweusi aliyepigania utu wa mtu mweusi?

BlackHistoryMonth.png
 
Back
Top Bottom