Hii ndiyo kampeni Mpya, Usiache kupiga kura

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,253
Reaction score
1,475
KAMPENI MPYA KWA MIAKA MITANO. Usichane kadi yako, usiape kutokupiga kura tena, Simama Kiume. Tanzania ni yako na sote tumeona upuuzi huu waliotufanyia?

1. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Hatutaondoa mabango ya Lowasa maeneo yetu ya kazi
2. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Tutatapeperusha bendera za chadema na ukawa kwenye magari, pikipiki na baiskeli zetu kwa miaka yote mitano ya kuvumilia dhuluma

3. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutahudhuria show yoyote au kununua kazi yoyote ya msanii aliyeshirikiana na CCM katika udhalimu huu. Pia hatutawapigia kura shindano lolote.

4. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutahudhuria function yoyote inayoitishwa na magufuli au waziri wake
5. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutajitokeza kwa mbio za mwenge, sikukuu ya uhuru wala msiba wa kiongozi wa CCM
6. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU raisi akifika kwetu tunajificha ndani aongee na aliokuja nao

7. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutapiga nyimbo za chadema, ukawa na mabadiliko kwenye magari na biashara zetu bila kusahau za wasanii ambao wamekuwa nasi katika safari hii.

8. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutasupport na kununua bidhaa za watu ambao walikuwa ukawa na wale amba hawakuwa upande wowote. Wale wa CCM uzianeni ninyi kwa ninyi mkiibiana muibiane huko.
9. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutatumia chombo chochote cha usafiri kilichowahi kuwa na bendera au chenye bendera ya CCM mafisadi na wavunjifu wa demokrasia

10. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutasalimiana ?MABADILIKO-LOWASA? NA ?LOWASA-MABADILIKO??.ambaye hataki afyate mkia.
11. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Magufuli akisikika kwenye redio au akionekana kwenye Luninga tunabadilisha channel

12. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutawapokea viongozi wetu wa ukawa hata ngazi ya serikali za mitaa kwa heshima, kama maraisi na mashujaa wetu. Wakija viongozi wa UKAWA tutaacha kazi zetu na kenda kuwasikiliza!

13. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutaendelea kusalimiana kwa vidole viwili hewani ili tusisahau juhudi zetu zilizominywa na wenye hela na mamlaka! Huu ndio mfungo na kilio chetu.

TUKINIA MAMOJA, HATA WALE WALIOACHA KURA ZAO ZIIBIWE HUKO VIJIJINI WATAAMKA TU! MIMI NAANZA LEO NA SITAACHA. HII NDIYO SAUTI YA WATU AMBAO CCM IMEWATUKANA, IKAWAPUUZA NA KUFANYA YAO
 
Si kwa nchi hii
Si kwa viongozi hawa wa ukawa
Si kwa wanachama hawa
Si kwa Watanzania ninao wafahamu
Tunahitaji uthibitisho wa kwanini Ukawa 2020 na si CCM
Tunahitaji uthibitisho wa Utakaothibitisha Watanzania waliopiga kura zaidi ya million 6 hawakufanya makosa
Muda wa kutegua kitendawili hiki ni miaka 5 tu majibu hadharani mbivu na mbichi tutazifahami
 
Wewe utakuwa unaumwa kifafa. Nadhani wewe ni kati ya wale waliolamba mafedha ya lowasa si bure.
Kwanza lowasa alishasema akishindwa anarudi zake Monduli kuchunga ngombe. Na wala hana haja sijui na uenyekiti wa chadema wala ukatibu. Kwanza alisema apata wasaa sasa wa kuendelea na matibabu yake kwa nafasi. Mlitaka kumuulia kwenye majukwaa washenzi kweli.
Hata mke wake Regina hataki biashara ya sijui ubunge wa viti maalum sijui nini. Naye anataka awe na muda wa kutosha kumuhudumia mumuwe. Biashata ya kukimbiakimbia na kina Mbowe imeputwa na wakati. Kiufupi yeye ukawa basii! ! Tafuteni mwingine.
Yooote uliyosema ni utumbo! Kwanza umebaki peke yako na mmeo na wanenu. wengine wote tumeshageuka zamani tunajenga nchi kuelekea uchumi wa kati. Hatutaki upumbavu wa kuchelewesheana muda hapa. Nchi nyingine wanakimbia sisi tunachechemea. Vipi? Tafakar chukua hatua
 
Si kwa nchi hii
Si kwa viongozi hawa wa ukawa
Si kwa wanachama hawa
Si kwa Watanzania ninao wafahamu
Tunahitaji uthibitisho wa kwanini Ukawa 2020 na si CCM
Tunahitaji uthibitisho wa Utakaothibitisha Watanzania waliopiga kura zaidi ya million 6 hawakufanya makosa
Muda wa kutegua kitendawili hiki ni miaka 5 tu majibu hadharani mbivu na mbichi tutazifahami

Tutawapima kwa ahadi mlizotoa!
 
Mi sitaashiriki zoezi la kupiga kura maishani mwangu hii kadi ntasajilia line mpya na tigo pesa
 
14. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU mtadeki barabara zote atakazopita Magufuli!
 
Acheni ulofa sasa ni kazi
Hayo maigizo pelekeni monduli
 
Khaa!!! wenye chama wanayafahamu haya au unaandika tuu??, Chapa kazi kiongozi uinue maisha yako na familia yako na taifa kwa ujumla. Wanasiasa hawaeleweki usishangae kwa miaka mingine mitano ukafanywa ndomu ukijakushtuka tayari umezeeka. Utachekwa hapa mjini
 
Wengine wanakimbia sisi tunachechemea kawa sababu ya serikali za CCM.
 
15. Kwa miaka mitano wabunge wetu hawatapokea posho ya walipa kodi wa Tz ambao wamechanganyika wa ccm cdm cuf act tlp
 
KAMPENI MPYA KWA MIAKA MITANO. Usichane kadi yako, usiape kutokupiga kura tena, Simama Kiume. Tanzania ni yako na sote tumeona upuuzi huu waliotufanyia?
1. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Hatutaondoa mabango ya Lowasa maeneo yetu ya kazi
2. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Tutatapeperusha bendera za chadema na ukawa kwenye magari, pikipiki na baiskeli zetu kwa miaka yote mitano ya kuvumilia dhuluma
3. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutahudhuria show yoyote au kununua kazi yoyote ya msanii aliyeshirikiana na CCM katika udhalimu huu. Pia hatutawapigia kura shindano lolote.
4. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutahudhuria function yoyote inayoitishwa na magufuli au waziri wake
5. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutajitokeza kwa mbio za mwenge, sikukuu ya uhuru wala msiba wa kiongozi wa CCM
6. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU raisi akifika kwetu tunajificha ndani aongee na aliokuja nao
7. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutapiga nyimbo za chadema, ukawa na mabadiliko kwenye magari na biashara zetu bila kusahau za wasanii ambao wamekuwa nasi katika safari hii.
8. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutasupport na kununua bidhaa za watu ambao walikuwa ukawa na wale amba hawakuwa upande wowote. Wale wa CCM uzianeni ninyi kwa ninyi mkiibiana muibiane huko.
9. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU hatutatumia chombo chochote cha usafiri kilichowahi kuwa na bendera au chenye bendera ya CCM mafisadi na wavunjifu wa demokrasia
10. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutasalimiana ?MABADILIKO-LOWASA? NA ?LOWASA-MABADILIKO??.ambaye hataki afyate mkia.
11. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU Magufuli akisikika kwenye redio au akionekana kwenye Luninga tunabadilisha channel
12. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutawapokea viongozi wetu wa ukawa hata ngazi ya serikali za mitaa kwa heshima, kama maraisi na mashujaa wetu. Wakija viongozi wa UKAWA tutaacha kazi zetu na kenda kuwasikiliza!
13. KWA MIAKA MITANO BILA VURUGU tutaendelea kusalimiana kwa vidole viwili hewani ili tusisahau juhudi zetu zilizominywa na wenye hela na mamlaka! Huu ndio mfungo na kilio chetu.
TUKINIA MAMOJA, HATA WALE WALIOACHA KURA ZAO ZIIBIWE HUKO VIJIJINI WATAAMKA TU! MIMI NAANZA LEO NA SITAACHA. HII NDIYO SAUTI YA WATU AMBAO CCM IMEWATUKANA, IKAWAPUUZA NA KUFANYA YAO

Umerogwa am a umetumwa?
 
Huo ndiyo ukweli anayekataa ni mtumwa.Mabadiliko daima.
 
Pia na wabunge wa ukawa wasichukue posho kwa muda wa miaka mitano
 
Nimekutana na vijana wengi ambao walipiga kura mwaka huu, wanahanikiza kwamba wao kwa kilichotokea kwenye Uchaguzi wa mwaka huu na kusababisha aliyekuwa Mgombea Urasi kupitia CHADEMA chini ya Mwamvuli wa UKAWA, E.N. Lowassa kushindwa uchaguzi huo, basi wao wanajiapiza hawatapiga kura tena maishani mwao.

Hili ni tatizo kubwa sana na wengine wao wamefikia kuzichoma au kuzichana chana kadi zao za kupigia kura. Lakini kuna majimbo UKAWA wamewashinda CCM kwa mbali sana, lakini jee tunadhani wana CCM kwenye majimbo hayo nao wanajiapiza kwamba hawatapiga kura tena maishani mwao na kuzichana chana kadi zao za kupigia kura au kuzichoma moto!?

Wazo la kuamini kwamba mwaka huu ndiyo ulikuwa mwaka pekee wa kuiondoa CCM madarakani si wazo sahihi. kwa wanaofuatilia siasa za nchi hii wanajua kabisa kuna hatua kubwa sana imepigwa na vyama vya upinzani kwenye uchaguzi huu. Niwaambie wale wanaojiapiza kutokupiga kura tena maishani mwao kwamba wazo lao hilo ni la kijinga kabisa na wanatakiwa walikatae!
 
Lowasa anasema haki yake imecheleweshwa ila haijapotea.
 
Back
Top Bottom