Wala haihitaji utafiti; walioipa CCM ushindi ni akina mama japo wachache wali-support opposition. Upinzani wanapaswa kujifunza namna ya kuwa-win wanawake wa rika zote. Sometimes "siasa za kistaarabu" hazilipi sana nchi hii. Bila kuchanganya "upumbavu" flani ambao ndio wengi wa hilo kundi wanaushabikia matokeo yataendelea kuwa hivyo hivyo miaka nenda rudi.
CCM wanajua sana kucheza na akili za makundi tofauti ya watanzania; wanajua namna gani "upumbavu" utumike ku-target kundi lipi na ni wakati gani busara itumike. Ni wakati gani "sasa ni zamu ya wanawake" i-apply, na ni wakati gani sio hivyo. Kwa akili zile nilizoshuhudia kwenye kampeni, kuenenda kwa busara na ustaarabu peke yake kwenye majukwaa ilikuwa kujitakia kushindwa.
Mkuu Magufuli na CCM ktk nafasi ya urais hawakushinda uchaguzi huu kupitia ballot box lakini ndiyo hivyo tena kishatangazwa "mshindi" and that's final na chapter imeshafungwa na jamaa ameshaapishwa na ameshaanza kazi!!
Kilichofanyika ni Tume ya uchaguzi kwa mamlaka ya kisheria na kikatiba yasiyohojiwa popote kumtangaza Magufuli mshindi!
Fahamu kuna "kushinda" kwa kupata kura nyingi kwa maana ya kupigiwa kura na watu wengi zaidi na kuna "kutangazwa" mshindi.
Na ili kuhalalisha tangazo la "kumtangaza mshindi" ni lazima aonekane ana idadi ya kura nyingi kwa namba kuwazidi aliowashinda!!
Hapa si hao vijana tu anaowasema mleta mada, isipokuwa karibu kila mtu amepigwa na butwaa hata asielewe ni nini hasa kimetokea!!
Ushindi wa Magufuli umehalalishwa vipi sasa? Tuendelee kusubiri labda na naamini tutaelewa tu huko mbeleni!!
Hivyo hoja ya wanawake hapa, binafsi sikubaliani nayo kwa sbb kwa uchaguzi wa mwaka huu sehemu kubwa ya jamii wanawake wakiwemo walikuwa tayari kwa mabadiliko ya kuiondoa CCM na walifanya hivyo!
Kikwazo ni mfumo wetu wa uchaguzi na sheria na katiba yetu.
Ni kweli hawa jamaa wana akili sana za kujihakikishia kuwa wanabaki madarakani kwa gharama yoyote ile na si kwa sanduku la kura au kwa eti kwa sababu wana ushawishi kwa wananchi especially kundi la wanawake kama unavyosema hapo juu, la hasha bali ni kwa kujitengenezea sheria za kuwalinda.
Angalia sheria ya mitandao (cyber crime act ya 2014), sheria ya takwimu, sheria ya uchaguzi na zingine nyingi ambazo wapinzani haziwapi nafasi ya kufurukuta. Hata sielewi Zanzibar kumetokea nini hadi CUF na Seif Shariff kuwazidi ujanja CCM!!
Nikubaliane kabisa na mleta mada kuwa suluhu si kukata tamaa wala kutupa ID zetu za kupigia kura, bali ni kukaa chini kutafakari ni nini kimetokea na tufanye nini huko mbeleni!
Binafsi kuna mama mmoja jirani yangu na kijana wa kiume tunaofahamiana kabisa wameapa kama alichokisema mleta mada kuwa hawatapiga kura tena kwa sababu tu waliyekuwa wanamtaka kashindwa. Nisichokuwa na uhakika nacho ni iwapo wameharibu ID zao za kupigia kura.
Lakini nimejaribu kuongea nao kuwaelimisha kuwa maisha hayako hivyo, huwa hatuanguki na kubaki umelala hapo bali unaamka na kuangalia sehemu uliyojikwaa na kisha unaendelea na safari mbele hadi mwishowe unafika ulipokuwa unakwenda!!