OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,046
- 114,510
Kama inavyoonekana kwenye Tovuti ya Bunge. Kamati ya Hali,Maadili na Madaraka ya Bunge ni Kamati iliyojaa CCM wakiongozwa na George Mkuchika ambao ni mmoja wa vigogo na makomredi wa chama.
Kama tunavyofahamu CCM kwa kubebana na kama tunavyofahamu wabunge wa CCM wanavyomhanya Rais Magufuli kiasi cha kuwakataza hata kuwasalimia wabunge wa upinzani wanapokuwa na matatizo. Na kama tulivyotanga ziwa pale Ubungo Flyovers kwamba hakuna wa kumpangia Magufuli.
Mimi sina imani na kamati hii,yenye wajumbe wanne tu toka upinzani. Kamati hii haiwezi "kumpangia" Rais kuhusu Makonda.
Maoni ya Kamati yanatakiwa yawe ni kuagiza/kushauri Rais atengue uteuzi wa Paul Makonda na sio vinginevyo