Uchaguzi 2020 Hii ndiyo hatma ya CCM na ukimya wa watu 7 wakubwa wa Membe

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
14,048
22,016
Naona wanachama wa CCM wenye roho ngumu wameamua kufunguka waziwazi kama kinachotokea hapa Dodoma kuanzia leo na kuendelea hasa wale wanaokatwa bila sababu za msingi.

Hali hiyo inaweza kuwafanya wakaja kuleta mapinguzi makubwa kutokana na ubaladhuli na nguvu inayoweza kutumika ndani ya week hii.

Picha iliyochanika leo ndiyo 'inayoweza' kutegemewa kwa wale watakaokatwa kwenye nafasi mbalimbali ndani ya chama kikongwe kinachodhaniwa kinaenda kupumzika muda mfupi ujao.

Futana na andiko
Siasa si lelemama kama baadhi yetu tunavyoangalia tukiwa nje, huko nje Tundu Antipas Lissu anachanja mbuga kila mkoa akitafuta wadhamini huku akiacha alama kutokana na hotuba zake, upande mwingine hatumsikii kachero mbobezi, mpatanishi na mshauri kimataifa Bernard K. Membe.

Moja ya kauli zake Ndugu, Membe ilikuwa kuna wanachama wanene/wazito saba (7) wapo nyuma yake, kwa sasa hawezi kuwataja kwa sababu anaogopa watafukuzwa kwenye chama, hao ndiyo watafanya mti mkubwa kuangushwa hali inayotufanya wafuatiliaji wa siasa kukaa kimya kusubiri, labda muda haujajiri.

Pamoja na hilo tunapata tashwishwi kujua je, bwana Bernard ana hofu ya kulimwa wakati wa kuwachuja au anasubiri Jumamosi ya tarehe 23.8 pale Dodoma ili kieleweke!

Yote kwa yote mbobezi anaonekana kalala usingizi wa mang'amung'amu na akiwatuliza wanaACT wenzake ili muda ufike waliamshe.
 
Jumamosi 23.08.2020 ndio itakuwa siku ya "KUJIHUKUMU" kwa CCM. Siku hio ndio itaamua ijizike au iendelee kujikongoja (Kwa kutumia dola).

Maana kuna "WANENE" wengi waliotia nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, ila wamecheza "FAULO" na wengine wamefunga "MAGOLI YA MKONO" wakati wa mechi ya kura za maoni na wakaongozea kwenye matokeo. Sasa watu wanasubiri "UADILIFU" wa refa kuangalia "VAR" na kama atawapa "KADI NYEKUNDU" ama laa.

Na kuna "WACHEZAJI CHIPUKIZI" pia walicheza faulo, ila mwisho wa mechi wakashindwa (Bashite), sasa wanasubiri "HURUMA" ya refa kuwabeba pasipo bebeka.

Patamu zaidi, na kuna kupitisha kikosi "1st ELEVEN" halafu mashabiki wakakikataa.

* Refa chonde chonde asije akawa ame "BET" katika mechi anayoichezesha mwenyewe. Wananchi watachana "MKEKA".
 
Jumamosi 23.08.2020 ndio itakuwa siku ya "KUJIHUKUMU" kwa CCM. Siku hio ndio itaamua ijizike au iendelee kujikongoja (Kwa kutumia dola)....
Hapo hapo tukumbuke wazito ambao hawakuingia hata 3bora wakiwemo mawaziri, rc nk wote hawa watakuwemo kwa filimbi ya refa wapende wasipende.
 
Ngoja tuone ni vigogo gani hao wakuwashinda waliohama mwanzo kama wakina Lowassa, Kingunge, Sumaye n.k.
watimkia ACT ama wapi.
 
Monduli mtoto wa Lowassa alishinda kura za maoni lakini JIWE kamkata kamrudisha Karanga eti kwasababu alihama Chadema kuja CCm hivyo apewe nafasi!!! Mkifanya hivyo huko Tunduma mtalia sana sana!!
 
Mtoto wa lowasa kakatwa?
 
Monduli mtoto wa Lowassa alishinda kura za maoni lakini JIWE kamkata kamrudisha Karanga eti kwasababu alihama Chadema kuja CCm hivyo apewe nafasi!!! Mkifanya hivyo huko Tunduma mtalia sana sana!!
Mambo kama hizi ndiyo zinaweza kuleta mapinguzi yanayoweza kuleta kumbukumbu hapa nchini, tusubiri muda.
 
Naona wanachama wa CCM wenye roho ngumu wameamua kufunguka waziwazi kama kinachotokea hapa Dodoma kuanzia leo na kuendelea hasa wale wanaokatwa bila sababu za msingi.

Hali hiyo inaweza kuwafanya wakaja kuleta mapinguzi makubwa kutokana na ubaladhuli na nguvu inayoweza kutumika ndani ya week hii.

Picha iliyochanika leo ndiyo 'inayoweza' kutegemewa kwa wale watakaokatwa kwenye nafasi mbalimbali ndani ya chama kikongwe kinachodhaniwa kinaenda kupumzika muda mfupi ujao.

Futana na andiko
Siasa si lelemama kama baadhi yetu tunavyoangalia tukiwa nje, huko nje Tundu Antipas Lissu anachanja mbuga kila mkoa akitafuta wadhamini huku akiacha alama kutokana na hotuba zake, upande mwingine hatumsikii kachero mbobezi, mpatanishi na mshauri kimataifa Bernard K. Membe.

Moja ya kauli zake Ndugu, Membe ilikuwa kuna wanachama wanene/wazito saba (7) wapo nyuma yake, kwa sasa hawezi kuwataja kwa sababu anaogopa watafukuzwa kwenye chama, hao ndiyo watafanya mti mkubwa kuangushwa hali inayotufanya wafuatiliaji wa siasa kukaa kimya kusubiri, labda muda haujajiri.

Pamoja na hilo tunapata tashwishwi kujua je, bwana Bernard ana hofu ya kulimwa wakati wa kuwachuja au anasubiri Jumamosi ya tarehe 23.8 pale Dodoma ili kieleweke!

Yote kwa yote mbobezi anaonekana kalala usingizi wa mang'amung'amu na akiwatuliza wanaACT wenzake ili muda ufike waliamshe.Mambweha mwaka huu watabwata sana ni mwendo wa ubatizo tu. Wale pension zama zilishapita fight against corruption is real with Magufuli no jokes.
 
Lile tetemeko limeenda kuvunja uchawi wa CCM..Lissu katoa kafara damu yake wao CCM wanachinja kondoo na mwenge haujawashwa mwaka huu..WAMEKWISHA
 
Hapo umeleta kitu kingine tena kwa wanasiasa wenye mlengo wa kafara hahahahaaaa...
 
Back
Top Bottom