Hii ndiyo Elimu bure!

Hii ndiyo Elimu bure!

Mkuu acha siasa za kinyesi ama za chooni.

Ina maana hiyo ndio picha pekee umeona ni majibu ya elimu bure?

Labda kama wewe ni mgeni hapa nchini tuseme umetoka somalia leo.

Unajitoa ufahamu na kujivika upunguani kana kwamba wewe ni kipofu wa kuona mwonekano mwanana wa miundombinu dhabiti ya shule zetu chini ya mpango wa ellimu bure ya mh Pombe?

Kwa akili yako tone ulitarajia serikali ishughulikie elimu tu huku secta zingine zisiguswe?

Huoni aibu kulaumu mabadiliko makubwa yanayofanywa na huyu mweshimiwa ambayo yumkini hakuna serukali yeyote huko nyuma imewahi kudhubutu ndani ya muda mfupi?


Chadema acheni siasa kinyesi.



Sent using Jamii Forums mobile app

Zimerudiwa Chaguzi za ajabuajabu baada ya watu kununuliwa- kwako haya ndo mambo mengine ya msingi unayoyasema?
 
Wakati anaachia ngazi, waziri mkuu mstaafu wa Uingereza Tony Blair aliulizwa:- Unadhani ni jambo gani linapaswa kutiliwa mkazo zaidi kuliko yote na waziri mkuu mwingine yeyote atakayekuja baada yako? Alijibu: EDUCATION, EDUCATION, EDUCATION (yaani elimu, elimu, elimu). Hebu fikiri:- Waziri Mkuu wa nchi iliyoendelea kama Uingereza na ambayo imekuwa inatoa elimu kwa watu wake kwa zaidi ya miaka elfu moja BADO ANAONA WATU WAKE WANAHITAJI ELIMU ZAIDI.

Sisi tunafikiri vitu vinavyoonekana ndio maendeleo kumbe bila watu wenye elimu hata tungekuwa na vitu vizuri namna gani ni bure. Vitatumiwa na viongozi waliosoma na matajiri na wageni lakini mwananchi wa kawaida havimsaidii. Kama vijana wetu hawana elimu bora ya sayansi, nchi yetu itakapokuwa nchi ya viwanda, hivyo viwanda vyetu vitaendeshwa na nani? Tunaweza kujihesabu kwamba tuna maendeleo makubwa kama kila jiji litakuwa na flyover kama ya Tazara na ya Ubungo n.k., na kuwa na barabara zenye njia nane kama zile za Singapore au China. Lakini, hayo ni maendeleo kwa wananchi wangapi maskini hapa nchini? Nadhani kuna haja ya kuangalia upya vipaumbele vyetu. Je, tunataka maendeleo ya vitu au ya vitu na watu pia?
 
Sema inaitwaje na iko wapi.

Kama ya kanisa tuwaulize pesa za kuendesha hizo shule wanapeleka wapi?

Vipi Mbowe watoto zake anasomesha wapi?

Ofisi mmeshajenga au bado mpo UFIPA?
Jibu Hoja Kwa hoja. Mbowe na familia yake wanahusishwaje na elimu ya ovyo. Hata kama uko serikalini sio lazima ujitoe ufajamu
 
Hapo ndiyo nnapowashangaa! Miaka ya kabla ya Uhuru mlijengewa mashule na kanisa. Serikali ina MoU na kanisa na pesa nyingi zinatolewa kila mwaka kupelekwa kanisani kwa ajili hiyo.

Sasa tufahamisheni, hiyo shule inayoongelewa kwenye post namba moja ni ipi?
Unawashangaa kina nani sasa,shangazi mimi nazungumzia kushindwa kwa serikali kujenga miundombinu ya kutosha ya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wake ilhali uwezo huo ilikuwa nao na inao,sasa mambo ya MoU ya serikali na kanisa yametokea wapi?.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm inaongoza kwa ushabiki.
Hapo hakuna kujali upande au chama unachoshabikia, jambo la msingi unapochangia mada au hoja jaribu kuelezea kwa kuangalia uhalisia na sii ushabiki sababu ushabiki haujengi
 
Watu wameng'ang'ania ishu za Mbowe as if Mbowe ndiye mwenye mandate ya kuendesha serikali!
 
Wazazi huko ni wazembe. Wanashindwa kufyatua Tofari na kujijengea madarasa?

Kulalamika vitu kama hivyo na mnasema Kagera ni wasomi inaonesha jinsi shule mlivyoenda kusomea ujinga.
kwani hiyo kodi wanayolipa ni kwa ajili ya matumizi gani? kila wakati kupitisha bakuli la kuwachangisha wananchi, uone aibu we ajuza siyo kisa unalipwa kwa kuendesha propaganda basi unalopoka tu.
 
Hii ndiyo elimu bure, watoto kusomea chini ya mti!View attachment 1013905

My take:

(1) Hela za kununua wapinzani na kurudia chaguzi zipo

(2) Pesa za kununua ndege kwa Cash bila mkopo zipo

(3) Pesa za kugawa mtaani kama njugu pindi mfanyapo ziara sehemu mbalimbali zipo

(4) Mnasema makusanyo yameongezeka na tuna mapesa mengi sana

(5) Pesa za Bunge Live hakuna, Pesa za Press Conference Live kila siku Magogoni zipo!

Wakati Pesa zote hizo zipo!
WATOTO WA WATANZANIA MASIKINI WANASOMEA CHINI YA MTI!

Hivi vipaumbele vyenu ni nini?



Unakosea, hii wilaya ina DED na mbunge.....jiulize wanafanya nini?
 
Back
Top Bottom