Hii ndiyo dini ya kweli namuomba Mungu anisaidie juu ya hili!!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Siku moja nilimtembelea rafiki yangu aliye kipofu. Kwa sababu ilikuwa usiku alifanya kitu kilichonifundisha sana. Nilipoingia ndani, Moses aliwasha taa. Nikamuuliza, Moses, kwa nini umewasha taa wakati wewe huoni?

Moses alicheka sana, akazima taa na kuelekea jikoni, kitambo kidogo akaja na chupa ya chai na mayai, akaviweka mezani kwa usahihi kabisa na akawasha tena taa.

Moses alichokisema kilinitoa machozi aliponiambia, Daudi!..... Sikuwasha taa kwa ajili yangu au kwa uhitaji wangu, ila kwa ajili yako wewe unayeona kwani wewe siyo kipofu kama mimi.

Halafu akaniuliza, "Daudi!! Ni mara ngapi umewazimia taa wengine ukiwanyima fursa ya kuona mwanga kisa tu wewe huuitaji?

Nilifikiri juu ya hilo kwa kina. Nami nakuuliza swali hilo leo, Ni mara ngapi umezima taa na kuwanyima wengine fursa ya kuona mwanga walipokuwa gizani???

Kwanini akaunti yako iwe na mamilioni huku mtoto wa ndugu yako akitembea bila viatu? Kwanini unatupa nguo usizovaa jaani wakati kuna anayekaribia kutembea uchi?

Kwanini vyakula vinaoza nyumbani kwako wakati kuna anayelala njaa?

Kwanini unaona fursa ya biashara na kuificha bila kuwashirikisha rafiki zako kisa wewe huihitaji?

Kwanini uko na nafasi ya kumsaidia mtu kupanda cheo au kupata ajira mpya hufanyi hivyo kwa sababu wahusika sii wa kabila lako au dini yako?

Kwanini unawachafua ndugu zako sababu hutaki mwingine awasaidie? Kila Swali Hapo Juu ni Sawa na KUZIMA TAA!!

Haya tuyaweke akilini kama Wanadamu. Tuanze kulenga yanayompendeza Muumba wetu na Ubinadamu. Hii ndiyo dini ya kweli, kuwasaidia wahitaji, wasiojiweza na wasiosikilizwa.

TAFADHALI WASHA TAA ULIZOZIMA! "Wewe ni nuru ya TAIFA LA MUNGU."
 
My nigga Tanzania ilinizimia taa since wayback na hawana mpango wa kuwasha.

Ni bumper to bumper
 
Hatujaumbwa kubebeana mizigo, jifunzeni kwa wadudu na viumbe wengine ambao sio compromised.
 
Back
Top Bottom