Kila kitu kipo ata usuchodhani hivi ushi kuna watu wenye roho kama hizi? Wapo

Ckeys

New Member
Apr 26, 2022
4
5
Siku moja nilimtembelea rafiki yangu aliye kipofu. Kwa sababu ilikuwa usiku alifanya kitu kilichonifundisha sana. Nilipoingia ndani, Moses aliwasha taa. Nikamuuliza, Moses, kwa nini umewasha taa wakati wewe huoni? Moses alicheka sana, akazima taa

Na kuelekea jikoni, kitambo kidogo akaja na chupa ya chai na mayai, akaviweka mezani kwa usahihi kabisa na akawasha tena taa. Moses alichokisema kilinitoa machozi aliponiambia, Daudi!..... Sikuwasha taa kwa ajili

Yangu au kwa uhitaji wangu, ila kwa ajili yako wewe unayeona kwani wewe siyo kipofu kama mimi. Halafu akaniuliza, "Daudi!! Ni mara

Ngapi umewazimia taa wengine ukiwanyima fursa ya kuona mwanga kisa tu wewe huuitaji? Nilifikiri juu ya hilo kwa kina. kumsaidia mtu kupanda cheo au kupata ajira mpya hufanyi hivyo kwa sababu wahusika sii wa kabila lako

Au dini yako Cyo watoto zako?
Kwanini unawachafua ndugu zako sababu hutaki mwingine awasaidie? Kila Swali Hapo Juu ni Sawa na KUZIMA TAA!! Haya tuyaweke akilini kama Wanadamu. Tuanze kulenga yanayompendeza Muumba wetu na Ubinadamu. Hii ndiyo dini ya kweli, kuwasaidia

TAFADHALI WASHA TAA ULOZOzima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom