Hii ndio "top ten" ya makabila yaliyoshikilia uchumi wa Tanzania

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
2,699
2,000
Moja kwa moja kwenye mada,ifuatayo ndio orodha ya makabila top ten yaani cream yaliyoshikilia share kubwa ya uchumi wa Tanzania.

1. Watu wenye asili ya asia wahindi, waarabu, wapemba nk

2. Wachaga

3. Wakinga

4. Wasukuma

5. Wahaya

6. Wanyakyusa

7. Wapare

8. Waha

9. Wamasai

10. Wakurya

Kama wewe unatokea makabila tofauti na hayo basi jitahidi kupata mwenza kutoka miongoni mwa hayo makabila Ili upige vita umaskini vinginevyo utamlaumu shetani bure.
 

Agresive

JF-Expert Member
Feb 18, 2018
471
1,000
Kuna ukweli wa makabila hayo lakini upangiliaje wake kinamba siyo sahihi hata kidogo.

Namba 8 hawajitangazi lakini ukifanya utafiti ni watu wamewekeza sana na wanafight sana katika biashara ingawa hawana tabia ya kuwekeza kwao. Kila mkoa mkubwa wenye mzunguko wa biashara hao watu wamejaa.

wahaya katika biashara sina uzoefu na hilo, zaidi tumewazowea katika elimu.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,413
2,000
"Katika karne ya 21 tunapanda basi la ukabila?"

Hayo sio maneno yangu ni maneno aliyowahi kuyatamka Mwl. Julius Kambarage Nyerere...

Huwezi kuamini nimegundua hapa kuna jamaa zangu na wadau nimekua nao wala sijui ni makabila gani (ila so long as issue zetu sio matambiko) nadhani haina tija....
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
721
1,000
Kabila langu hapo lipo lina nina uhakika ambao hawajatajwa hapo wengine maisha yao ni mazuri maradufu kuliko yangu mimi niliyetajwa! Hapo ndipo unapaswa kujiuliza, kama na mwenzangu kabila lako lipo hapo juu, sasa je wewe mwenyewe binafsi, au angalau wazazi wako, uchumi wenu unaakisi na ulichokiandika?!
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
2,699
2,000
Kabila langu hapo lipo lina nina uhakika ambao hawajatajwa hapo wengine maisha yao ni mazuri maradufu kuliko yangu mimi niliyetajwa! Hapo ndipo unapaswa kujiuliza, kama na mwenzangu kabila lako lipo hapo juu, sasa je wewe mwenyewe binafsi, au angalau wazazi wako, uchumi wenu unaakisi na ulichokiandika?!
Jifikirie mara mbili mbili
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,616
2,000
3. Wakinga/Wabena

Wajita na wajaluo🤔🤔
wakinga na wabena🤔🤔

Yani kwa akili yako nahisi umeona kwasababu hao watu ni majirani nasi ukaamua kuwaweka kundi moja, hapa ebugi mkuu

Mbena naye umeona kweli kumuweka level za mkinga?? umeona kwasababu wote wanatokea njombe ndio uwaweke kundi moja ? kuwa siriazi aisee, Mbena kweli ndio umeona umuweke hii list ya top 10 ya wanaoshikilia uchumi ???

Mjaluo naye umeona kumuweka namba moja na mjita, kwa kipi mjaluo kashikilia uchumi wa nchi? hapa umerudia kosa lile lile la kumpachika mbena kwa mkinga kisa ni majirani, kumbuka mtu anaweza kuishi karibu na matajiri lakini yeye akawa sio tajiri.

ila hatuwezi jua, huenda kwako baba mjaluo mama mbena ukaona utafute kambinu na wewe ujimwambafai 😂
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
2,699
2,000
Sioni cha kufikiria mara mbili mbili hapo kwa sababu makabila yote hayo uliyotaja, majority ya watu wake ni maskini wa kutupwa! Nitakuwa mjinga nionee ufahari utajiri wa mtu mwingine ambae si mzazi wangu na wala sina undugu nae wowote
Kwanini asiwe wako au usiwe wewe? Mkuu hayo makabila kuna watu wenye nafuu zaidi ya maisha kuliko makabila mengine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom