Uchaguzi 2020 Hii ndio Tanga ya Rais Magufuli (2015 - 2020)

jijiletublog

Member
Jul 23, 2020
31
125
UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TOKA UGANDA MPAKA TANZANIA

Rais Yoweri Museveni na Raisi JPM wamezindua ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki kutoka wilaya ya Hoima, nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, nchiniTanzania. Bomba la mafuta lenye joto, ambao ni refu zaidi duniani, litagharimu dola bilioni 3.5 na ujenzi wake utakamilika mwaka 2020 ambapo Uganda itajiunga na kundi la nchi zinazozalisha mafuta. Ujenzi wa bomba la mafuta utafanywa na Total E&P, CNOOC na Tullow Oil pamoja na serikali mbili za Uganda na Tanzania. Bomba la mafuta litakapomilika litasafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa kila siku.

Gharama ya kusafirisha pipa la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga itakuwa dola 12.2 kwa pipa, na kuyafanya mafuta ya ghafi ya Uganda kuwa na faida hata kwa kiwango cha leo cha dola 50 kwa pipa.

Rais aliyaomba mataifa yote ya Afrika Mashariki kulichukulia bomba la mafuta la Afrika Mashariki kama mali ya Afrika Mashariki, akibainisha kuwa kwa kugundulika kwa mafuta na gesi katika nchi nyingine katika eneo hilo, bomba litakuwa chombo cha kusafirishia mafuta kuelekea baharini kutoka nchi zote za Afrika Mashariki.

Kwa mafuta kuja Tanga, Tanzania sasa itanunua mafuta ghafi kutoka Uganda badala ya kuingia gharama kubwa za kuagiza kutoka nchi za Kiarabu, huku Uganda pia itaiuzia mafuta Tanzania kwa gharama nafuu. Tanzania pia itapata ujuzi na utaalamu kutoka kwa wataalamu wa Uganda ambao watakuwa na uzoefu katika sekta ya uchimbaji mafuta. Aliwahimiza makandarasi ili kuhakikisha kuwa wanakamilisha mradi kwa muda unaotakiwa, akisema kitu chochote kinyume cha hapo kitaleta sifa mbaya kwao na kwa nchi zao

UMEME
SAT, chini ya uogozi wa raisi JPM imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwa wakazi wa mkoa wa tanga katika vijiji na miji. Mkoa mzima una vijiji 518 vilivofikiwa na huduma hii wakati hapo awali ni vijiji 175 tu vilivyokuwa na huduma hii. Vijiji 261 pekee ndio vimesalia ambavyo vinategemewa kumalizika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Raisi magufuli anastahili miaka mitano tena aweze kumaliza tatizo hili. Tanzania nzima ina vijiji 12228, kati ya hivyo, 9700 vimekwishafikiwa na huduma ya umeme. Ni vijiji vichache vilivyosalia. Raisi JPM apewe muda Zaidi ili huduma hii iweze kufika sehemu zote za nchi yetu.

BARABARA
SAT, chini ya uongozi wa raisi magufuli imeweza kujenga barabara ya kutoka Tanga mjini mpaka Pangani yenye urefu wa km 50 kwa gharama y ash bilioni 66.8. imefanikiwa pia kujenga barabara ya kutoka muheza – amani yenye urefu wa km 40. Mbali na hayo, SAT, imefanikiwa kujenga barabara nyingi tanga mjini Pamoja na kujenga stand ya kisasa ya korogwe na soko la kisasa kwa gharama ya shilingi bilioni 39.9 pamoja na kukarabati barabara ambazo zina jumla ya urefu wa km 3494. Hii yote ni kumrahisishia mfanyabiashara na mtanzania wa kawaida kujikwamua kutoka katika shida za usafiri zilizokuwepo hapo mwanzo.

ELIMU
Ndani ya miaka mitano, SAT imetumia gharama za sh bilioni 55.7 kwa ajili ya fidia ya elimu bure, ambapo kati ya hizo, bilioni 17.8 zimetumika katika kujenga miundombinu ya elimu na kukarabati na kuboresha shule za mkoa wa Tanga. SAT imefanikiwa kujenga shule za secondary 228 na za msingi 905 nchi nzima ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma ya elimu na kila mtoto aweze kupata elimu kama ilivyo haki yake.

AFYA
Kwa kipindi hiki cha miaka mitano, jumla ya sh bilioni 17.4 zimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa dharula na jengo la kuchuja damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya mkoa wa Tanga. SAT, chini ya uongozi wa raisi JPM imefanikiwa pia kujenga hospitali mpya tano, ambapo hospitali tatu zipo katika wilaya za korogwe, tanga jiji na muheza na tayari zimekamilika na zinatoa huduma. Hospitali mbili zilizopo katika wilaya ya handeni na mkinge bado zinaendelea kujengwa. Sasa kuna jengo jipya la wazazi atika hospitali ya lushoto na X-ray za kisasa Bombo, Lushoto na Korogwe. Serikali imefanikiwa kujenga vituo vya afya 22 na kuviwezesha kufanya upasuaji wa dharula. Zahanati tano mpya pia zimejengwa kuwapunguzia wananchi wa tanga kero ya kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya na hivo kupunguza vifo vya mama na mtoto.

MAJI
Ndani ya miaka mitano, miradi 64 ya maji imetekelezwa katika mkoa wa tanga ambapo miradi 54 ni ya vijijini na 10 ni ya mjini. Mradi wa maji kutoka pongwe-muheza umejengwa kwa gharama za sh bilioni 3.07 ila na unatarajiwa kusambazwa vijijini, ikiwa umefika asilimia 85 hadi sasa. Mradi wa maji wa mabokweni uliogharimu sh bilioni 2.4 umefanikiwa kupita mleni, kibafuta, mpirami, naoya na chongoreni. Miradi mingine ni kama ule wa sume, manolo na madala uliogharimu sh bilioni 2.64 pamoja na miradi mingine mingi. SAT, chini ya uongozi wa raisi magufuli inampango wa kuanzisha mradi mwingine wa maji kutokea mto Pangani utakaogharimu bilioni 200. SAT inaahidi kutimiza miradi mingine ya maji mkoani tanga ili kufikia 95% ndani yam waka 2021.

IMG-20201020-WA0332.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom