Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
CHADEMA hawana mshikamano wala ushirikiano kama taasisi ndani na nje bali wana baadhi ya viongozi wachache sana ambao wana uwezo mkubwa katika kuzicheza siasa za Tanzania huku wakisaidiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo hata kama CHADEMA isingekuwepo yangetokea.
Jaribu kuangalia historia ya Tanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii kupata picha halisia ili ikusaidie kujenga hoja mbadala kujua siraha kuu ya CHADEMA.
Hata swala la kuwepo kwa katiba halijaanziswa na CHADEMA kama unavyotaka kuaminisha watu hapa JF.
Siraha kuu ya CHADEMA siyo mshikamano na ushirikiano bali ni KUWEPO kwa CCM na serikali yake madarakani kwa muda mrefu ambao umeweza kujenga LUNDO la maswali yasiyo na majibu mbadala, makosa kiutendaji kwa maksudi au kutokujua na chama na serikali kuishi kwa mazoea.
Mambo haya mpaka yamesababisha wananchi katika maeneo mbali mbali kuwachagua viongozi wa vijijini, madiwani na wabunge kutoka vyama vya upinzani ambao hawana hata uwezo ukilinganisha na wale wa CCM. UJUMBE hapa kutoka kwa wananchi ni kusema, TUMECHOKA tunataka wengine tofauti bila kujali UWEZO WAO.