JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,383
- 9,829
- Thread starter
- #41
Kuna matatizo ni vyema kufanya diagnosis na kuona live data. Ila hivi wapo mafundi kweli hapa ambao wanaweza kusoma live data na kuzielewa ama ndio kusoma code basi mchezo umeisha? Maana kuna matatizo mengine bila live data utajikuta umepigwa chenga.
Sijajua.. Ingawa nimeshakiona kitu kimoja kwamba unakuta kaenda kupima kaambiwa hamna tatizo lolote kwa sababu tu hakuna code iliyodisplay.
Wakati kama huyo anayepima angezipitia live data angeweza kujua baadhi ya shida. Sababu live itakuambia kama hewa inayopita ni kidogo, kuna kuna mahali kuna leak kupitia fuel trims, Itakuambia rpm ni kiasi gani, joto la coolant ni kiasi gani, n.k. Na kutoka kwenye hizo data unaweza kujua mbivu na mbichi.