Hii ndio sababu kwanini sitaki kukopa benki

Hii ndio sababu kwanini sitaki kukopa benki

Kijana kijana

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
2,546
Reaction score
2,624
Wakuu vuteni picha robo tatu ya mshahara wote nakopea naenda kununua kiwanja na tofali pesa inaishia..

Halafu wakati kabla sijakopa ile pesa kamili ya mshahara ilikuwa haitoshi kwa mahitaji yangu ya msingi,..alafu eti nichukue ile ile ambayo haitoshi naipunguza kwa kwenda kujengea alafu sina biashara sina chochote,..wadai hii kweli imekaa powa pesa ya kukopa nikajengee?

Sawa ni rasilimali waweza uza anytime lakini inakuwa haina maana ukiwa na njaa uuze kiwanja bwana.

Wafanya kazi wengi kwa utafiti wangu tunaishi maisha magumu kwa sababu kile ambacho hakitoshi tunaenda kukikopea na kuuzika ule mkopo katika sehemu ambayo haizalishi pesa ya kila siku na huku hamna chanzo kingine cha mapato.

Sasa matokeo yake ni kwamba mshahara unakuwa hautoshi mara tatu yake aise halafu mbaya zaidi ile robo tatu unayopokea unalipia madeni na huku ukiwa na uwanja wako mzuri unasubiri mda uishe ukope tena ...

Aiseeee mfanyakazi wiki ya kwanza kupokea mshahara anakula kuku, wiki ya pili ataanza kula watoto wa kuku(mayai) wiki ya tatu ataanza kula chakula cha kuku(mahindi au ugali)

Wiki ya nne sasa anakuwa kuku hasa mana sio kwa kuzurura huko...

Leteni maoni wadau ni upi mpango sahihi wa kukopa pesa ili kuhakikisha mkopo haitufishi njaa.
 
Duu, Mimi nilishaacha kukopa benki siku nyingi.

Njia nzuri ni kuhakikisha unajitahidi kuweka akiba japo kidogo katika kile unachokipata na kupanua fikra zaidi za kuongeza kipato chako kwa njia halali.

Pia jaribu kupunguza au kuacha matumizi yasiyo na tija mkuu.
 
Duu, Mimi nilishaacha kukopa benki siku nyingi.

Njia nzuri ni kuhakikisha unajitahidi kuweka akiba japo kidogo katika kile unachokipata na kupanua fikra zaidi za kuongeza kipato chako kwa njia halali.

Pia jaribu kupunguza au kuacha matumizi yasiyo na tija mkuu.
nashkuru mkuu...
kumbe ni bora ukaendelea kuchukua vilaki sita vyako bila kukopa huku ukijipanga na akiber ya kutosha
 
Kabisa mkuu, hata mbuyu ulianza kama mchicha. Na Ujenzi hautakiwi ukufanye uishi maisha ya tabu na dhiki, ingawa kujibana ni muhimu. Jenga kwa phases utashangaa mjengo umeisha bila kupata maumivu. Zingatia vipaumbele vyako mkuu, kila la kheri.
 
wakuu vuteni picha robo tatu ya mshahara wote nakopea naenda kununua kiwanja na tofali pesa inaishia..

alafu wakati kabla sijakopa ile pesa kamili ya mshahara ilikuwa haitoshi kwa mahitaji yangu ya msingi,..alafu eti nichukue ile ile ambayo haitoshi naipunguza kwa kwenda kujengea alafu sina biashara sina chochote,..wadai hii kweli imekaa powa pesa ya kukopa nikajengee?

sawa ni rasilimali waweza uza anytime lakini inakuwa haina maana ukiwa na njaa uuze kiwanja bwana,..

wafanya kazi wengi kwa utafiti wangu tunaishi maisha magumu kwa sababu kile ambacho hakitoshi tunaenda kukikopea na kuuzika ule mkopo katika sehemu ambayo haizalishi pesa ya kila siku na huku hamna chanzo kingine cha mapato...

sasa matokeo yake ni kwamba mshahara unakuwa hautoshi mara tatu yake aise..alafu mbaya zaidi ile robo tatu unayopokea unalipia madeni na huku ukiwa na uwanja wako mzuri unasubiri mda uishe ukope tena ...

aiseeee...mfanyakazi wiki ya kwanza kupokea mshahara anakula kuku,
wiki ya pili ataanza kula watoto wa kuku(mayai)
wiki ya tatu ataanza kula chakula cha kuku(mahindi au ugali)

wiki ya nne sasa anakuwa kuku hasa mana sio kwa kuzurura huko...


leteni maoni wadau ni upi mpango sahihi wa kukopa pesa ili kuhakikisha mkopo haitufishi njaa...
karibuni wadau
Endelea kutuwekea hizo pesa sie wanaume tukachukue tuzifanyie kazi..
 
Kabisa mkuu, hata mbuyu ulianza kama mchicha. Na Ujenzi hautakiwi ukufanye uishi maisha ya tabu na dhiki, ingawa kujibana ni muhimu. Jenga kwa phases utashangaa mjengo umeisha bila kupata maumivu. Zingatia vipaumbele vyako mkuu, kila la kheri.
asante sana..

ilitosha comment zako iwe mwisho wa uzi mkuu..
njoo huku tuliko mkuu..mtu anakopa milioni tano alafu hyo yote ananunua uwanja kisha anasubiri mkopo uishe ili akope tena akapige foundation........ aiseee
 
Mimi nlishakopa benki mbili tofauti kile kilikuwa kipindi kigumu sana kwakweli. Nikamaliza mkopo mmoja ukabaki mmoja wa standard chatered huo ndio ulikuwa balaa mwisho wa siku kuupunguza makali ikabidi niuhamishie NBC ulivyoisha 2016 nikasema sirudii tena kukopa na kweli Mungu kanisaidia sijapata dharura ya kukopa benki tena...bora mikopo ya kazini aisee ingawa hupewi hela nyingi lakini ukiwa na dharura inasaidia....nakushauri ukope benki kama kote kwingine imeshindikana na hiyo hela unahitaji kupita maelezo
 
asante sana..

ilitosha comment zako iwe mwisho wa uzi mkuu..
njoo huku tuliko mkuu..mtu anakopa milioni tano alafu hyo yote ananunua uwanja kisha anasubiri mkopo uishe ili akope tena akapige foundation........ aiseee
Duh! Hatari sana!
 
Kopa nunua Shamba, alaf litumie shamba kujipatia mkopo zaidi na kuanzisha kilimo au ufugaji utatoka. Njia nzuri ni kukopa kwa malengo ya kuzalisha pesa zaidi sio kwa ajili ya kujenga au kununua Gaari
 
Back
Top Bottom