Hii ndio mbinu nayotumia kwenye biashara

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,039
Kama ume plan kufanya biashara Fulani then ukafanya hesabu ukakuta inahitaji 1milioni na wewe unakihasi hicho cha Pesa usianze na mtaji kamili cha kufanya chukua laki tano anza hivyo hivyo kwa tabu ili kujua biashara inachangamoto gani au inahitaji uongeze mtaji kwenye sehemu ipi ya biashara,kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi ya wewe kusoma biashara zaidi kuliko kuanza na mtaji wote,pia itakuwa rahisi pia kubadili gia angani ukiona biashara hiyo imekukataa,biashara haitegemei Sana mtaji Bali biashara inategemea mzunguko,mfano unaweza ukawekeza 1milioni halafu ukawa unafanya mauzo sawa na yule aliyewekeza Laki nne!niishie hapo kwa leo
 
Kichwa cha uzi na uzi wenyewe havina uhusiano.sasijui ni uelewa wangu mdogo au ww umeshindwa kujielewa na kutuelewesha pia!!sijui
 
Mkuu, umeandika jambo la msingi sana. Kuna mtu unaweza kukuta ana mtaji wa milioni mia na anaweka milioni mia zote, biashara ikimkataa anarudi kijiweni tayari ameshafirisika
 
ni vizuri kama biashara huna uhakika nayo yani unasitasita lakini kama biashara unailewa na plan zako umeziweka vizuri why uanze kwa mtaji pungufu usiojitosheleza.
 
ni vizuri kama biashara huna uhakika nayo yani unasitasita lakini kama biashara unailewa na plan zako umeziweka vizuri why uanze kwa mtaji pungufu usiojitosheleza.
Lakini mimi jamaa nimemuelewa hii inasaidia pale unapotaka kuanzisha biashara yapili tofauti na unayofanya
 
Back
Top Bottom