barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Nimeambatanisha picha tatu,picha mbili zinamuonesha Dr Shein akiwa Serena Hotel kumjulia hali Jongwe Maalim Seif,wale wazee wa "body language" wanaweza kuona "uso" wa Dr Shein na ule wa Maalim Seif.Jongwe Maalim akimkazia macho Dr Shein,lkn katika picha zote mbili Dr Shein hamtazami usoni(machoni) Jongwe wa siasa za upinzani Zanzibar.Picha husema mara 1,000 zaid ya maneno.
Wakati Mwanyekiti wa CCM Zanzibar akimua kuonyesha uungwana na ubinadamu na kumtembelea ndugu Maalimu Seif kumjulia hali juu ya afya yake,Maskani kuu ya CCM maarufu kama "Maskani ya Kisonge" imeandika Ujumbe tata sana katika ubao wake.Ubao huu unafahamika na kusifika kutumika kuandika maneno ya kejeli kwa wapinzani wa CCM Zanzibar.
Safari hii ujumbe unaonekana kulenga afya ya kiongozi wa upinzani wa CUF,hali hii inakatisha tamaa,wakati mwanyekiti akiwa Dsm kuonyesha upendo walioko Zanzibar wanaendeleza chuki na lugha za kuudhi.Maadhimisho ya Muungano yaligubikwa na mabango ya lugha za kibaguzi na CCM kuomba radhi,Je hili bango la Kisonge halina chembe cha chuki na lugha ya kuudhi?
"When The Sultan of Zanzibar drums,All great Lake Regions Dance"