KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 30,220
- 69,335
Mwaka 1984 Ronald Reagan akiwa rais wa 40 wa U.S,kwa muunganiko wa bunge na viwanda alipendekeza kuundwa kwa space station ambayo hapo awali jambo hili lilionekana kama nadharia!(science fiction) mbele za watu!.
Baada ya ushawishi wa rais Ronald Reagan,u.s ilikubali jambo hilo nakuamua kuanza mikakati ya kutengeza iss,lkn U.S haikutaka kuwa pekee bali ilikaribisha nchi nyengine zipatazo 15 ktk kuunda na kutumia ISS...
U.S na URUSI wameonekana kuwa na mchango mkubwa ktk kufanikisha uundwaji wa chombo hicho ambapo ktk mwaka 1998 rocket ya kirusi ilioneka ikipasua anga kwaajili ya kupeleka kipande cha kwanza cha ISS.
Hii inamaanisha ISS ilitengenezwa kwa vipandevipande kisha kupelekwa angani kwenda kuungwa na kuwa kitu kimoja,miaka miwili mbele ISS ikawa tayari kwa watu kuitumia ambapo tarehe 2 november 2000...