Leo nimepita Ubungo mataa nikaona kuna askari wa upepelezi (waliovalia kiraia)wanakamata boda boda na kuwanyanganya funguo kwa ajili ya makosa madogo madogo ambayo ni ya kupewa onyo tu!Lakini wanasumbuliwa hadi utawahurumia.Cha kushangaza ni kwamba kulikuwa na askari waliovaa kiraia kama 30.Hivi kweli hii nguvu inayotumika kwa hawa vijana wanaojitafutia riziki kwa nini isitumike kuzuia uhalifu na hao majambazi wanaoua raia na polisi?au nchi imefilisika hadi tulipwe mishahara kwa faini za boda boda?