Hii ndio elimu ya bongo - Case Study Ardhi University na UDOM

PowerWithin

JF-Expert Member
Mar 8, 2014
651
500
Wanajamvi!

Tuanzie Ardhi University:

Kuna Programme inaitwa Bsc in Information Systems Management. Ni program ya miaka 3.

Sifa za kupata:
Two principal leve passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Physics, Geography, Chemistry, Economics or Computer Science.

==========================================================

Twende UDOM:

Kuna Programme inaitwa Bsc in Information Systems. Ni programme ya miaka 3

Sifa za kupata:
Two principal level passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Geography, Physics, Chemistry, Economics, Accountancy, or Commerce.

Twende UDOM tena usichoke:

Kuna programme inaitwa Bsc in Business Information Systems. Inasomwa miaka 3.

Sifa za kupata:
Two principal level passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Georgraphy, Physics, Chemistry, Economics, Accountancy, or Commerce.

Programme hizi ki ukweli hazina tofauti kubwa sana katika contents zake. Ninachokiona ni kuwa UDOM wapo kisasa zaidi kwa kuweka Accountancy na Commerce kama kigezo cha kupata mojawapo ya programme zao hapo juu.

KWA MWAKA HUU:

Kwa mujibu wa jamaa yangu aliye apply, Ardhi wamemkataa applicant wa Bsc in ISM aliyesoma PCB A level akiwa na pass zifuatazo. Physcics - D, Chemistry - D, na Biology - D. Na kama haitoshi ana ADVANCED DIPLOMA IN ACCOUNTANCY yenye GPA ya 3.5.

Na wamemwandikia sababu ya kukosa kuwa ni kukosa minimum requirement inayohitajika, il hali kwenye profile yake NACTE/TCU wamemwandikia Required Qualification found. Kuna selected applicant kwa mwaka jana alichaguliwa na Ardhi kusoma Bsc in ISM akiwa amesoma A Level HGL.

Huyu wa PCB kwa mtazamo wangu sidhani kama ana sifa ya kukosa kwa kuambiwa minimum requirement not met, labda angeambiwa stiff competition ningeweza kuelewa. Lakini tusubiri second selection ya Ardhi tuone kama kuna watu wenye pass kubwa zaidi yake.

Hapa kuna vitu viwili vinaibuka tofauti: TCU/NACTE wanakuandikia Required Qualification found, na hao hao wanakuambia minimum requirement not met kama kigezo cha kutochaguliwa. Kuna mwingine ana GPA ya 4.5 ameandikiwa Minimum requirement not met. Aiseee mbona pasua kichwa hii kitu. Na hii ndio nchi yetu safari bado ni mbali sana.

MY TAKE:

Mimi kwa mtazamo wangu binafsi nilidhani jamaa huyu ambaye tayari ana elimu ya mambo ya biashara ni mzuri sana ku intergrate na elimu ya masuala ya teknolojia. Kwangu namwona kama ni Asset kwa Taifa kuamua ku sacrifice miaka 3 kusoma teknolojia huku tayari akiwa na elimu ya biashara.

Hawa ndio wanaokuja baadaye kutengeneza software za ukusanyaji kodi maana kodi anaijua na teknolojia anaijua. Hawa ndio wanaokuja baadaye kutoa ushauri wenye maana katika kufanya uchumi wa nchi kuwa wa kisasa/kiteknolojia maana uchumi na teknolojia anaujua.

Lakini nchi yake haioni hilo. Kitendo cha kusoma Accountancy ambayo kimsingi ni hesabu ingemtosha kuipiku Economics na Mathematics iliyowekwa kama kigezo cha kupata Bsc in ISM. Lakini katemwa. Kaambiwa hana minimum requirement.

Ikumbukwe kuwa programme hio hata ajira yake ni sawa na kusema HAIPO maana ni kweli haipo. Ni kubaingaiza tu. Dunia ya sasa ni biashara na teknolojia. Na nadhani UDOM wameona hilo na wakaweka Accountancy/Commerce kama kigezo mojawapo cha kusoma Information Systems kwenye chuo chao. Na hapa ndipo notion ya kuwa UDOM ni chuo cha kisasa kinashika hatamu.

Kuna thread iliwahi kuletwa humu ndani ikiwaponda UDSM kwa suala la Paschal (wale wa Computer Engineering/Science). Napata shaka kuwa huenda hivi vyuo vyetu kongwe vya umma nchini vinashindwa kwenda sambamba na kasi ya kiuchumi na teknolojia katika ulimwengu wa kisasa. Wanashindwa kutengeneza 'Intergration'.

Kwa miaka kadhaa ijayo Dunia itashuhudia UDSM wakibobea kwenye research na kupata sifa nyingi huku vyuo kama UDOM, RUAHA, TEKU, KAMPALA na vingine vingi vikiendelea kuwatoa wahitimu mahiri kwenye fani mbalimbali zinazoakisi uchumi wa kisasa na teknolojia ya kisasa.

Ni hayo tu.
 
Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,526
2,000
Good! Vyuo vikongwe vijiangalie UDOM inakuja juu sana na ni tishio kwa vyuo vikongwe ndiyo maana kinapigwa vita sana
 
harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,890
2,000
Kwa kweli umejitahidi kuweka sawa hapo nimeona jinsi ambavyo umeweka vigezo vya kutosha .

Ulinganifu Wa kiwango chake kwa vyuo vyote viwili ni nzuri bila haijalishi lazima watakupa sababu tu ila hizo sababu hazina maana kwamba ndio vitakuridhisha wewe.

Wote Wa natamani kupata wanafunzi Wa kutosha ila ukiona wanawaacha jua nafasi haitoshi tu .
 
sime

Senior Member
Jul 14, 2016
146
225
Wanajamvi!

Tuanzie Ardhi University:

Kuna Programme inaitwa Bsc in Information Systems Management. Ni program ya miaka 3.

Sifa za kupata:
Two principal leve passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Physics, Geography, Chemistry, Economics or Computer Science.

==========================================================

Twende UDOM:

Kuna Programme inaitwa Bsc in Information Systems. Ni programme ya miaka 3

Sifa za kupata:
Two principal level passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Geography, Physics, Chemistry, Economics, Accountancy, or Commerce.

==========================================================

Twende UDOM tena usichoke:

Kuna programme inaitwa Bsc in Business Information Systems. Inasomwa miaka 3.

Sifa za kupata:
Two principal level passes (minimum 4 points) in any of the following: Mathematics, Georgraphy, Physics, Chemistry, Economics, Accountancy, or Commerce.

==========================================================

Programme hizi ki ukweli hazina tofauti kubwa sana katika contents zake. Ninachokiona ni kuwa UDOM wapo kisasa zaidi kwa kuweka Accountancy na Commerce kama kigezo cha kupata mojawapo ya programme zao hapo juu.

KWA MWAKA HUU:

Kwa mujibu wa jamaa yangu aliye apply, Ardhi wamemkataa applicant wa Bsc in ISM aliyesoma PCB A level akiwa na pass zifuatazo. Physcics - D, Chemistry - D, na Biology - D. Na kama haitoshi ana ADVANCED DIPLOMA IN ACCOUNTANCY yenye GPA ya 3.5.

Na wamemwandikia sababu ya kukosa kuwa ni kukosa minimum requirement inayohitajika, il hali kwenye profile yake NACTE/TCU wamemwandikia Required Qualification found. Kuna selected applicant kwa mwaka jana alichaguliwa na Ardhi kusoma Bsc in ISM akiwa amesoma A Level HGL.

Huyu wa PCB kwa mtazamo wangu sidhani kama ana sifa ya kukosa kwa kuambiwa minimum requirement not met, labda angeambiwa stiff competition ningeweza kuelewa. Lakini tusubiri second selection ya Ardhi tuone kama kuna watu wenye pass kubwa zaidi yake.

Hapa kuna vitu viwili vinaibuka tofauti: TCU/NACTE wanakuandikia Required Qualification found, na hao hao wanakuambia minimum requirement not met kama kigezo cha kutochaguliwa. Kuna mwingine ana GPA ya 4.5 ameandikiwa Minimum requirement not met. Aiseee mbona pasua kichwa hii kitu. Na hii ndio nchi yetu safari bado ni mbali sana.

MY TAKE:

Mimi kwa mtazamo wangu binafsi nilidhani jamaa huyu ambaye tayari ana elimu ya mambo ya biashara ni mzuri sana ku intergrate na elimu ya masuala ya teknolojia. Kwangu namwona kama ni Asset kwa Taifa kuamua ku sacrifice miaka 3 kusoma teknolojia huku tayari akiwa na elimu ya biashara.

Hawa ndio wanaokuja baadaye kutengeneza software za ukusanyaji kodi maana kodi anaijua na teknolojia anaijua. Hawa ndio wanaokuja baadaye kutoa ushauri wenye maana katika kufanya uchumi wa nchi kuwa wa kisasa/kiteknolojia maana uchumi na teknolojia anaujua.

Lakini nchi yake haioni hilo. Kitendo cha kusoma Accountancy ambayo kimsingi ni hesabu ingemtosha kuipiku Economics na Mathematics iliyowekwa kama kigezo cha kupata Bsc in ISM. Lakini katemwa. Kaambiwa hana minimum requirement.

Ikumbukwe kuwa programme hio hata ajira yake ni sawa na kusema HAIPO maana ni kweli haipo. Ni kubaingaiza tu. Dunia ya sasa ni biashara na teknolojia. Na nadhani UDOM wameona hilo na wakaweka Accountancy/Commerce kama kigezo mojawapo cha kusoma Information Systems kwenye chuo chao. Na hapa ndipo notion ya kuwa UDOM ni chuo cha kisasa kinashika hatamu.

Kuna thread iliwahi kuletwa humu ndani ikiwaponda UDSM kwa suala la Paschal (wale wa Computer Engineering/Science). Napata shaka kuwa huenda hivi vyuo vyetu kongwe vya umma nchini vinashindwa kwenda sambamba na kasi ya kiuchumi na teknolojia katika ulimwengu wa kisasa. Wanashindwa kutengeneza 'Intergration'.

Kwa miaka kadhaa ijayo Dunia itashuhudia UDSM wakibobea kwenye research na kupata sifa nyingi huku vyuo kama UDOM, RUAHA, TEKU, KAMPALA na vingine vingi vikiendelea kuwatoa wahitimu mahiri kwenye fani mbalimbali zinazoakisi uchumi wa kisasa na teknolojia ya kisasa.

Ni hayo tu.

Hivi hii Bsc.Information System Management ni kama Bsc.Computer Science?, Maana sijaona prospectus ya Udom nijue contents/Modules zake, Brother .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom