Hii ndio dunia tunayoishi

Hii ndio dunia tunayoishi

NASRI1

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2019
Posts
210
Reaction score
284
Ukiilewa dhana ya dunia halisi tunayoiishi kwa sasa wanadamu basi itakusaidia kuijua vema nafasi yako kama
mwanadamu na namna sahihi ya kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuenenda na kasi ya dunia yetu ya
sasa.

Kwanza ni vema ukijua ya kwamba tunaishi katika dunia ya kisasa ambayo inaipa akili nafasi ya kufanya kazi
ngumu kwa niaba ya mwili, yaani ni dunia ambayo kichwa kinatakiwa kifanye kazi ngumu ili kuunusuru
mwili.

Ni dunia ambayo dhana ya *Darwin* (survive for the fittest) kwamba ni watu imara tu ndo wenye nafasi ya
kuendelea kuwepo inajidhihirisha kwa mapana, kwa sababu ni dunia ambayo makosa yako, shida zako na
uzembe wako ni mtaji wa mwingine kuelekea mafanikio yake.

Tupo katika dunia ambayo dhana ya upendo sio tena kitu kinachokuja kwa asili (naturally) bali ina vichocheo
vyake vingi kikubwa kikiwa ni ziada ya uwezo na utashi binafsi wa mwanadamu husika.

Kuporomoka kwa upendo wa asili miongoni mwa wanadamu kumezaa dunia ya watu wabinafsi, wenye choyo,
chuki na kila aina ya roho mbaya na wenye kujitazama wao zaidi bila kujali wangap wataumia na kwa kiasi
gani kupitia hiyo mitazamo yao binafsi.

Ni dunia ambayo kuenenda na kasi yake inahitaji akili ya ziada inayochochewa na utashi wa kuyakubali
mabadiliko ya kimazingira na kimfumo. sio dunia ya kusubiri furaha kutoka kwa mwanadamu mwenzio, ni
dunia ya kuitafuta furaha yako kwa nguvu zako na matarajio yako mwenyewe.

Ni dunia ambayo unaweza hata kufanya biashara na adui wa rafiki yako kwa maana rafiki wa adui yako sio
lazima sana awe rafiki yako, rafiki yako ni yule tu mwenye kuenenda na fikra na matarajio yako bila kujali
matarajio yako yanawaumiza wangapi na kivipi.

Hamasika.
 
Back
Top Bottom