Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Si fan wa huyu kijana Nnauye, na inathibisha kiuwezo wake wa maamuzi sio competent ya kuwa na title aliokuwa nayo na ndio maana huwa miongoni mwa few wanaomake big headlines for wrong reasons. Lakini nimpongeze kwa juhudi zake alizochukuwa kujisomesha na kuweka kipaumbele katika elimu yake. Ni mfano mzuri kwa vijana wasiokata tamaa katika kujiendeleza kielimu kwa future zao.

Kusoma ni nyenzo katika uongozi, lakini sio kigezo pekee cha uongozi, wapo waliokuwa ni viongozi bora huku wakiwa na elimu ndogo, uongozi ni talent ambbayo sio kila mmoja wetu atakuwa nayo, hivyo elimu pekee isiunganishwe na kipaji cha uongozi.
 
Nape maelezo so shallow weka grades huongei na laymen hapa ni wasomi tunaokuzidi fahamu hilo, so be deteiled
 
Miaka hiyo Butimba waliendesha mafunzo ya jioni kwa elimu ya sekondari.Mbunge mpina ni miongoni mwa waliofaidi elimu hiyo kama Nape
 
:llama:Butimba T.T.C hakuna Advanced secondary level! Au alifanya Mtihani kama private Candidate? Oyaa! Punguza kutumia Mataputapu kabla hujaleta maada yoyote humu!
 
Alisoma EGM katika Chuo cha Ualimu Butimba? Chuo cha uamili wanasoma waliotoka kidato cha nne au cha sita kuanzia madaraja ya 3 hadi ya nne (nne nzuri si karibu na ya mkia).

Sasa yeye Butimba kuna A-Level au chuo cha ualimu? Naomba kuelewesha hapa?

Diploma inasomwa mwaka mmoja? Kama ni ndivyo certificate unasoma muda gani? Kudadeki hana kitu huyu!! Hivi si alipata division iv ya point 29 o=level?

Naomba kusahihishwa hapa!! Ninachojua ni bomu kichwani ila siasa za uswazi anaziweza!!
 
Miaka hiyo Butimba waliendesha mafunzo ya jioni kwa elimu ya sekondari.Mbunge mpina ni miongoni mwa waliofaidi elimu hiyo kama Nape

Basi ni bora kusema kuwa hakupata credit cha kumtosha kuingia direct kidato cha sita kwa hiyo alifanya private candidate!! Huyu alipata division iv o-level!!!
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu “3” kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika “thesis” iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)

Shabanii, IKO TAKA KAZI? :A S shade:
 
Wizi mtupu mwanzoni mlituambia kasoma advance butimba,wakati pale kuna chuo cha ualimu na o-level tu leo tena mnasema nsumba???? Tujadili matatizo yetu TZ nasio cv ya nape ambayo haimsaidii kitu mtanzania anayekufa kwakukosa huduma muhimu e.g Dawa,maji,chakula,elimu bora n,k
 
Ushauri wa bure kwako na huyo Nape aliyokuandikia hiyo CV chovu:
1. Mkajifunze jinsi ya kuandika CV
2. Unatoa usifa wa matokeo ya darasa la saba, mbona kimya kwa matokeo ya form 4 na 6 kama ni masafi kweli?
3. Popote pale ukiona mtu mwenye vyeti vya kuunga unga level moja (diploma-diploma) huyo ni mbumbu.
4. Degree za India tunazijuwa sana, vigezo vya kujiunga VETA hapa bongo ni vya juu kuliko vigezo vya kujiunga na vyuo vya India ambavyo wabongo wengi mnavikimbilia. Ukiwa na 'zero' secondary unapata admission ya chuo huko mara moja, na hakuna kufeli alimradi uwe unalipa ada.
5. Masters gani hiyo ya Mzumbe pamoja na Thesis yake ambayo umeweza kupata chini ya Mwaka mmoja-usilete danganya toto za siasa hapa
6. Nataka kumsikia Nape kwenye kongamano au mkutano wowote ndani au nje ya nchi akito mada (presentation) kwa 'English' kama tulivyo kwisha wahi kumsikia Mnyika au Zitto-Ndipo jamii ipime kwanza uwezo wako wa kujieleza na kuchanganua issues, na siyo mambo ya propaganda hapa za vua gamba
7. nakuachia kiporo
 
Nape maelezo so shallow weka grades huongei na laymen hapa ni wasomi tunaokuzidi fahamu hilo, so be deteiled

Punguza tambo mkuu! No human being pefect at all! Pamoja na kiburi chako chote cha elimu, but neno "deteils" ulilolitumia haliko sawa!
Hakuna neno la kingereza kama hilo!
Hujaitendea haki lugha unayojidai nayo!
Nway sisi wenye elemu ndogo tumeelewa ulitaka kuandika nini !
 
CV ya kihuni iliyoandikwa na muhuni mwenzake, tunachotaka sisi ni O-level, alipata alama zipi na A-level alipata zipi, mbona mnyika kaeleza, au ana Gentleman bachelor degree aliyepata wakili wangu Ridhiwani kikwete. Hakika wasomi makanjanja
 
Too late to comment, but for sure this man is very weak. Mbona ana elimu ya kujifunika na vyeti saana kuliko kuelimika. Wa namna hii PhD zenu kama za faza Rizi1
 
Dah Nape umejiaibisha sana, unaanzisha ugomvi wa mawe kwenye nyumba ya vioo? anyway nangoja vita kati ya sugu na mh. Mulugo manake naskia mheshimiwa :tape2:anatumia vyeti vya mtu.
 
Habari wana JF,
Mtoa mada amejaribu kuandika kwa niaba ya Nape, ambapo Nape mwenyewe hajaona haja ya kuandika. Ni labda Nape mwenyewe anajua maswali yatakayozaliwa hayana majibu yaliyonyooka sawa au majibu yaliyopo siyo matamu kuyatoa hadharani. Hata hivyo bado kuna machache ambayo binafsi, bila unafiki ningependa kupata ufafanuzi hasa kutoka kwa Nape mwenyewe(ikiwezekana)

1.Inaonekana muda wa elimu ya msingi na sekondari Nape alihamahama sana. Binafsi najua hii inaweza kuchangiwa na mzazi kuhama kwa sababu zozote. Lakini pia inaweza kutokana na shule kushindwa kumvumilia mwanafunzi kutokana na kushindwa kufikia viwango vya ufaulu au kuwa na nidhamu isiyoridhisha. Ni kwa nini ilikuwa hivyo kwa Nape?

2. Hizi diploma za mwaka mmoja nadhani zilitakiwa kuwa vyeti(Certificaetes) tu..Sioni ni vipi unaweza kusema ulisoma diploma namna hiyo.Naona ingekaa vizuri kama hizi tungeziacha pembeni tu.

Inasemekana (na waliosoma naye) kuwa vipindi fulani perfomance ya Nape haikuwa sawa (hasa kule India) hili likoje? Nafikiri aliyeandika anaweza kusema pia Nape alipata nini wapi, ikiwezekana maoni ya anafikiri ni kwa nini.

Mwisho naomba niseme tu kuwa Ni bahati mbaya kwamba mambo tunayosoma Shuleni na vyuoni huwa hayako applicable sana katika system za maisha halisi duniani. Wakati mwingine elimu uliyo nayo inaweza isichangie sana kukufanya kuwa mtu bora. Zaidi itategemea malezi, makuzi na busara binafsi katika kukubali kuongozwa na KWELI au HALI HALISI. Kwa haraka nakusudia kusema MTU YEYOTE NI ZAO LA MFUMO ULIOMUANDAA!
 
Back
Top Bottom