Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ni Mtoto Wa Kwanza katika Familia ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne. Ambapo Kijana huyu Mwenye Moyo wa Huruma,upendo , unyenyekevu na ukarimu Alizaliwa Tarehe 16-4-1979 katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
ELIMU: Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete Alianzia masomo yake ya shule ya Msingi huko Mkoani Lindi maeneo ya Nachingwea katika shule ya msingi MATANGINI Mwaka 1987. Mnaweza kujiuliza ni kwanini alianzia shule ya msingi huko Mkoani Lindi?
Jibu ni Kuwa Kijana huyu aliyekaa Miezi Tisa na Aliyezaliwa kutoka Tumboni Mwa Mama Afahamikae kwa Jina La AZIZA .Jina Ambalo Pia Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete Amempatia Mwanae wa kwanza au waweza kusema Binti yake wa kwanza . Ambapo waweza kusema Jina la mtoto wa kwanza wa Ridhiwan ni la Mama yake mzazi Ridhiwani Mwenyewe Yaani AZIZA. Kwa hiyo Aziza Ridhiwani ni jina la Bibi Yake.
Sasa Embu turejee sababu za Ridhiwani kuanzia shule ya msingi huko Mkoani Lindi. Sababu ni Kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa anafanya kazi na amepangiwa kazi mkoani humo kama katibu wa CCM wa wilaya. Na hapa unaweza kupata connection ya vipi alikutana na kuoana pia na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete Ambaye ni First Lady wetu mstaafu japo kwa sasa ni Mbunge kule Mjengoni Dodoma Katika Bunge linalokwenda kuvunjwa Ijumaa hii na Mama yetu kipenzi sana Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Hapa natamani ningewapa kastori kidogo ka namna Mama Salma Kikwete Rafiki kipenzi wa Mama Mwantumu Mahiza walivyokutana mpaka kuoana na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Lakini kwa leo naomba nijkite kwenye CV ya Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete Pekee.
Embu tuendelee. Hata hivyo baada ya kuanza shule ya msingi hapo Nachingwea,mwaka mmoja baadae Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete na wazazi wake walihamia Mkoani Mtwara na hivyo kumbidi kuhamia huko Masasi katika shule ya msingi MKOMAINDO . Lakini pia haikupita muda mrefu Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alirejea na kuhakia Dar na wazazi wake na kwenda kumalizia Masomo yake katika shule ya Msingi Forodhani.
Elimu ya secondary: Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete alisoma Katika shule ya Sekondari Ya Shabaan Robert . Hii ni shule maarufu sana hapa nchini hususani katika jiji la raha ,jiji lenye kutumia akili nyingi ,jiji lenye kila aina ya tabia ,jiji la starehe ,jiji pendwa ,jiji ambalo ni ndogo ya kila mtanzania kufika hapo . Hapa namaanisha Dar es salaam . Hapa ndipo mtoto huyu wa jakaya Kikwete na mkewe AZIZA alisoma masomo yake ya O Level .
.
Lakini baadaye Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete Aliendelea na masomo yake katika shule ya secondary Mkwawa inayopatikana mkoani Iringa . Ambapo kwa sasa shule hii ni chuo kikuu cha Elimu Tawi la UDSM ambalo lina matawi matatu yanayotoa shahada ya Elimu . Ambapo lingine ni DUCE.
Baada ya kutoka kwenye ardhi hii ya shujaa wetu Mkwawa aliyewachakaza wajerumani mpaka akamuua Kamanda wao zelewsk. Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete Aliendelea na Elimu ya juu katika Chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kama UDSM au waweza kusema Mlimani. Chuo kinachobeba vipanga,chuo kinachobeba wanafunzi wenye ufaulu wa juu,chuo kilicho na historia ndefu ya Nchi hii,chuo kilichotoa marais wawili wa Taifa letu na mawaziri wasiohesabika ,chuo ambacho ndio nembo ya Taifa letu katika Elimu.
Chuo ambacho Ukifika pale unahisi upo Harvard university au yale university Marekani au oxford au Cambridge university UK huko.
Hapo Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete alisajiliwa kusoma masomo ya sheria katika kitivo cha sheria. Kitivo ambacho ili uweze kusajiliwa na kupata nafasi hapo ni lazma uwe umepata alama za juu sana tena sana . Ni lazima uwe akili kubwa na siyo akili za kukariri na kumeza madesa na kuyaimba kama kasuku. Hapo ni lazima uwe na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo na siyo kurapurapu tu utafikiri mwana hipapu aliyelewa gongo..
Ambapo Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete aliweza Kumaliza masomo yake vizuri kabisa na kwa ufaulu mzuri sana tena sana .akiwa chuoni hapo nyota yake ilikuwa ikiwaka sana ambapo alichaguliwa katika nafasi mbalimbali kama vile mwenyekiti wa kitivo cha sheria ,mbunge ,katika wa Daruso yaani Daruso kwa wale ambao hawajapitia hapo udsm maana yake ni serikali ya wanafunzi. Ambapo inakuwa na Rais wake ,mawaziri na kila kitu. Na ina bajeti yake kabisa
Ambapo chuoni hapo Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete aligeuka kuwa kama Dhahabu au lulu kwa namna alivyokuwa mtetezi wa wanafunzi na maslahi yao mpaka kuonekana kama mtetezi wa wanyonge na sauti ya wanafunzi wote. Aliwasaidia sana wanafunzi mbalimbali bila kiburi.alikuwa msikivu sana kwa kila mtu na alifikika kwa urahisi sana na kila mtu mwenye shida alipewa nafasi ya kusikilizwa na kusaidiwa.
Ndugu zangu nitaendelea wakati mwingine maana CV ya Mheshimiwa ni ndefu sana na huwezi kuimaliza kwa siku moja. Na ukianza kuisoma mbele za watu napo pia huwezi kuimaliza . Naomba nipumzike kidogo kwa sasa maana hata kichwa kinauma na akili imechoka. Ana CV nzito na ndefu kuliko hata barabara kuu ya Dar hadi Tunduma.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.