Hii ndio bei mpya ya mafuta Zanzibar

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
01 (2).jpg
MAMLAKA
ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo itaanza kutumika kesho Jumanne 13/03/2018. Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Hassan Juma Amuor amesema kuwa ZURA imetangaza bei mpya kwa kuzingatia mambo yafuatayo.

Alisema kuwa wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani,thamani ya shilingi ,gharama za usafiri ,kodi za Serikali pamoja na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Aidha alisema kuwa bei hizo Petroli kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi moja(1)kwa lita kutoka shilingi 2,256 hadi kuwa shilingi 2,257 sawa na ongezeko la asilimia 0.04%.

Bei ya mafuta ya Dizeli kwa mwezi wa Machi .2018 imepanda kwa shilingi(68)kwa lita kutoka shilingi 2,175 hadi kuwa shilingi 2,243 sawa na asilimia 3%.

Pia Afisa Uhusiano huyo alisema bei ya Mafuta ya taa kwa mwezi wa Machi.2018 imepanda kwa shilingi (5) kwa lita kutoka shilingi 1,641 hadi shilingi 1,646 sawa na ongezeko la asilimia 0.3%. Vilevile alisema kuwa bei ya mafuta ya Banka kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi (68) kwa lita kutoka shilingi 2,017 hadi shilingi 2,085 sawa na ongezeko la asilimia 3%.

Hata hivyo alisema kuwa bei ya Mafuta ya Ndege (Jet A-1) kwa mwezi wa Machi 2018 imeshuka kwa shilingi 4.46 kwa lita kutoka shilingi 1,811.80 hadi shilingi 1,807.34 sawa na upungufu wa asilimia 0.24%.


Muungwana
 
Yaani bei ya wese zenji ni sawa na bei za Canada! Dah bongo nyoso. ..kwa kipato gani hicho jamani? Acheni kuwaua wananchi. Jamani!
 
Kumbe katika huu mkoa gharama za maisha ziko juu......nitaendelea kukaa mkoa wa kyela. Petrol ya Malawi 1500
 
Back
Top Bottom