Hii nchi yetu ni ya hovyo sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii nchi yetu ni ya hovyo sana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ulukolokwitanga, Mar 14, 2012.

 1. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wametutaka tu update taarifa za akaunti zetu za benki. Leo nikaamua kuanza hilo zoezi kwa akaunti zangu zote tatu. Cha kustaabisha benki zote tatu zinahitaji taarifa zinazofanana kwa kutumia fomu tofauti, which means unapanga foleni tatu tofauti kuwasilisha taarifa ambazo almost the same.

  Wakati naprocess leseni ya udereva niliwapa hizo taarifa TRA, wakati naprocess passport niliwapa hizo taarifa Uhamiaji na nikisafiri nje jamaa huwa wana scan airport or bank or hotelini wanakuta data zote.

  Ajabu ni kwamba hapa TZ hakuna taasisi inayoshugulika na takwimu, idara ya taifa ya takwimu imejifia kifo cha mende. Profile yangu ni ile ile, sijawahi kubadili jina kama Mwigulu Nchemba, kwa nini mnihangaishe kujaza mifomu kila kukicha badala ya kuwa na centralized database ambayo watu wa bank, TRA, uhamiaji na wengine waifuate idara ya takwimu wakiihitaji mimi niwe na update tu?? Viongozi wa CCM mmeshindwa kuleta maendeleo inakuwaje mnashindwa kuwa na vitu vidogo kama takwimu?

  Najua mnatake advantage kwa kuwa takwimu sahihi zitawazuia kufanya ufisadi kwa kuandikisha majina ya marehemu kwenye makampuni yenu ya kifisadi lakini dunia ya sasa imebadilika na nyie mbadilike kwa maendeleo ya taifa. Leo nimejuuuuta kuwa na akaunti
   
Loading...