Hii mvua ya Dar sasa imezidi sifa

Hii mvua ya Dar sasa imezidi sifa

Kama hiyo mvua inaua watu na kuharibu miundombinu, ina maana mungu anaileta iue watu ili viumbe wengine wapone au waishi?

Mfano mvua iliyonyesha hivi majuzi msumbiji na kuua watu zaidi ya 1000, je mungu aliileta iue watu ili viumbe wengine waishi?
Je unajua hiyo hiyo mvua kwa kunyesha hivyo mola ameokoa maisha ya viumbe wangapi?? Ukilinganisha na idadi ya hivyo vifo
 
Hii mvua inayonyesha Dar sasa imezidi. Hizi ni sifa za kijinga.

Huko vijijini hainyeshi inatuletea shida hapa mjini.

Huwezi kutoka kwena mahala muda wote ni mvua tu.

Watu tumekosa hata muda wa kwenda kujipanga barabarani kuupokea mwili wa mzee wetu Mengi.

Ikanyeshe huko vijijini watu waivishe mazao. Hapa mjini mvua tumeichoka.
Hapo unamlalamikia nani mkuu??
 
yaani wewe unaakili sana kuliko aliyekuumba? unampangia mungu kazi za kufanya. wewe na mkuu wa mkoa wa tabora naona mpo sawa alisema mungu ndie amshukuru rais sio rais amshukuru mungu.unajua sababu ya mvua kunyesha hata hapa mjini nia ya mungu ni nini au unafikiri mvua mungu anaileta kwa kilimo tu.kasome quraan mungu kaeleza anateremsha mvua kwa ajili ya kitu gani utaona sio kilimo pekee kuna wadudu wadogo wapo kwenye ardhi joto linawaumiza wanahitaji maji na unyevuunyevu ili uhai wao uendelee ndege anahitaji mvua ardhi nayo inahitaji maji ili ipate uhai
 
Hivi ndivyo baadhi ya binadamu wasivyokuwa na akili kukufuru mchana mpaka usiku.

Kwani nani alikuambia ujenge makazi sehemu yenye kupokea mvua nyingi? Kama hutaki mvua nyingi si uende mikoa isiyo na hizo mvua nyingi? Embu tutolee balaa.
 
Kila kitu kiwe na kiasi. Kama kitu kinaleta maafa na madhara makubwa hicho sio kitu kizuri. Hata biblia inasema kila kitu kiwe na kiasi.

Haiwezekani limvua linajinyeshea tu toka asubuhi hadi kesho asubuhi.
Aibu sana kuwa na watu wenye akili kama yako na unajikakamua kuinukuu Bibilia bila aibu huku ukikufuru. Ungekuwa huamini uwepo wa Mungu ningekuelewa.
 
Aibu sana kuwa na watu wenye akili kama yako na unajikakamua kuinukuu Bibilia bila aibu huku ukikufuru. Ungekuwa huamini uwepo wa Mungu ningekuelewa.
Kwani kuna mahala nimekwambia naamini?
 
Daslama nguo zisipokauka vizuri inakuwaga shida ukiziweka ndani zikakutana na joto tena kama huziwek poa zinavunda zinakuwa na hatufu mbaya, mvua leo itukaushie kidogo, daaaah
 
Hapo unamlalamikia nani mkuu??
Mkuu simlalamikii mtu but I just wanted to get some things out of my chest, it is a kind of relief.

Sure wiki hii nina mipango mingi ya hela nzuri sasa hii mvua inataka kuharibu mambo. Ikanyeshe huko vijijini. Huku hatulimi na miundombinu yetu ni mibovu mitaro imeziba, mitaro finyu, ujenzi wa hovyo hovyo na mambo kama hayo. Huku ni kero zaidi ya furaha. Ikanyeshe huko watu wanalima.
 
Hivi ndivyo baadhi ya binadamu wasivyokuwa na akili kukufuru mchana mpaka usiku.

Kwani nani alikuambia ujenge makazi sehemu yenye kupokea mvua nyingi? Kama hutaki mvua nyingi si uende mikoa isiyo na hizo mvua nyingi? Embu tutolee balaa.
Kukufuru ndio kufanyaje?
 
Je unajua hiyo hiyo mvua kwa kunyesha hivyo mola ameokoa maisha ya viumbe wangapi?? Ukilinganisha na idadi ya hivyo vifo
Kwani haiwezi kunyesha ambayo itaokoa viumbe na pia isisahabishe maafa? Ni lazima iharibu sehemu moja ili kuokoa sehemu nyingine?
 
Binadamu Hana shkrani
Ikiwepo jua kali lawama
Ikiwepo mvua lawama
Sasa ngojeni siku mletewe kimbunga tsunami mchezo nalo

Ova
Kweli sisi binadamu ni viumbe wa ajabu sana juzi tu hapa waumini na viongozi wa dini wamekesha wakiomba mvua imeanza kunyesha tunaanza lawama.
Kwa style hii tunakoelekea Mwenyezi Mungu atatuchoka.
 
😂😂😂 nna mababy wawili sasa hivi mmoja bado yuko hukoooo mmoja ndio huyu mtu mzima mwenzangu yupi unamsemea?
Poleni sana msalimie baby ukiongea naye.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jangwani pamefungww magari yanaelekezwa njia mbadala
 
Back
Top Bottom