Hii Mikoa Nani Kailoga?

Barabara ya kibiti - Lindi, Masasi(Mangaka)-Tunduru-songea...........miaka 50 ya Muungano hakuna kinachoeleweka........na Bado watu wa huko mtakoma........kwani huko ni TZ......? mpaka Rais ajaye atamaliza muda wake na ataziacha barabara hizo bila kukamilika.......Tunashugulikia mambo ya kitaifa kama vile Gas, Uranium, makaa ya mawe, Pembe za Ndovu............
 

Na huo ndo ukweli! Hakuna mkoa hata mmoja, narudia hata mmoja ambao unamiundombinu mizuri halafu tukadanganywa kuwa wananchi walichangia kufanya miundombinu kuwa bora!
 
Kuna mikoa ilihujumiwa kwa sababu za chuki za dini ukabila pamoja na uwezo mdogo kimapato kwenye kuchangia pato la taifa
 
Hapo mtwara tandahimba kuna dogo langu lilichaguliwa form five.. Likashndwa na maisha...

Tandahimba haina shule hata mmoja ya A level labda ianze mwaka huu.. Acha kutuuzia ubuyu hapa ebu tutajie jina la shule.
 

Na sio wilaya hizo tu Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara ina NMB, CRDB na NBC pia kuna mamlaka yake ya maji haitegemei MTUWASA inayo MANUWASA inayoshughulikia Masasi na Nachingwea kwa upande wa Radio hata Clouds na fm radio kule ina masafa yake pamoja na Nachingwea tofaut na Mikoa mingine radio zipo makao makuu tu ya mkoa.
 
Kama wajanja katika utafutaji mali wamekimbilia Dar, unategemea huko nani atapaendeleza?

Kama dar kuna wajanja wangekimbilia Ulaya na South unategemea Bongo nani ataendeleza. Watu kuhamia sehemu fulani ni kutafuta fursa kwaajili ya maendeleo yao na walikotoka ndo maana hata wachaga wametoka kwao moshi kuja jijini ingawa kwao hakuna dhiki kihivyo.
 
Ee baba......! tunakuomba uwape macho na uwezo wa kuona na kuipa kipaumbele cha maendeleo mikoa yetu ya KUSINI, kwa uwepo wa GESI na MAKAA YA MAWE vitubadilishe kweli kimtazamo, kielimu na uchumi.
 
kiukweli mikoa ming tanzania kwa upand wa vijijini hali hazitifautiana xana coz nimejionea ruvuma,iringa, mbeya, mtwara, morogoro, dodoma xo tucidangabywe eti ni mtwara vijijini tu ndo hali mbaya

Nature ya kazi zangu imenifanya kuzunguka mikoa mingi hapa nchini, karibia 80%, na hasa vijijini. Nimefanya kazi Lindi na Mtawara about 7 yrs ndo maana nimeizungumzia mazingira magumu waliyonayo wananchi hawa. Kuna vijiji unaenda unaweza kuhesabu nyumba za bati, ukionyeshwa maji ya kunywa hutaweza kuamini kama ni maji ya kunywa mwanadamu. Vijumba vingine milango ni ya makuti tuu na imeegeshwa , habari ya choo ndo usiseme,. Ninakwambia haya kwani nimeshiriki kazi za TASAF 1 kuibua miradi, Miradi ya mazingira n.k kwa hiyo tumezunguka sana kwenye vijiji hivi. Huwezi ukalinganisha Kijiji kilichopo Mtwara au Lindi na vijiji vya mikoa kama Morogoro.
 
<p><br type="_moz">mi nahisi kwa sababu hawana zao kubwa la biashara pia mwingireza hakuwahi weka makazi huko ndo maana inakuwa ngumu kuendelea tofauti na mikoa mingine walijengewa mpaka rami</p>
 
Safi mkuu, haihitaji PHD kujua hali ya maisha ya sehemu flani na hivi ndio vigezo vyetu vya kawaida kabisa vya kuangalia kama mji umeendelea au vipi maana ukikuta sehemu kuna taasisi za fedha zaidi ya tatu ujue hapo mzunguuko wa fedha ni mzuri na ndio maana commercial bank kama CRDB au NBC zimetia timu. Pia kuna ofisi ya NSSF hapo Masasi na ni wilaya chache sana hazizidi 15 zenye ofisi ya NSSF
 
Kweli mkuu, kama mtu hujapita kwenye vijiji na miji mbalimbali unayoyasema mtu hawezi kuelewa, ni kweli vijiji na sehemu nyingi haina tofauti lakini kuna sehemu zingine zinahitaji awareness tu kidogo watu wabadilike ila kuna zingine zinakuwa hoi though kwa observation unaweza kuona kama zipo sawa lakini ukiziingia kiundani kuna ambazo zipo hoi kinoma
 
Kuna mikoa ilihujumiwa kwa sababu za chuki za dini ukabila pamoja na uwezo mdogo kimapato kwenye kuchangia pato la taifa
Kama Tabora, kwa historia yake ilitakiwa iwe imepiga hatua sana lakini ndio hivyo tena mpaka leo ipo ipo na ukifanya masihara Nzega itakuwa mkoa mwingine kwa jinsi inavyokua. Tabora nadhani ilihujimiwa kutokana na kwamba tangu enzi za utemi ilikuwa haitawaliki pia tulivyopata uhuru wapinzani wengi wa mkulu wa nchi wa enzi hizo walikuwa wanatoka Tabora pamoja na kwamba nchi ilikuwa changa (nawaza kwa sauti lakini)
 



Umewatukana waasisi wa uhuru.
 
Umewatukana waasisi wa uhuru.
Samahani mkuu, nilikuwa nafanya tathimini ndogo nikilinganisha contribution ya mkoa wa Tabora before na after Uhuru nikilinganisha na mikoa mingine michache ambayo sserikali imefanya investment kubwa kupita kiasi kuliko contribution ya mkoa husika katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kuisahau kabisa mikoa ile iliyochangia pato la taifa kupitia Tumbaku, Asali na mazao mengine i.e. tunatakiwa tuikumbuke ile mikoa ambayo ipo hoi lakini ile mingine iliyoonyesha uhai nayo tuirudishie shukrani kwa mchango wao (mambo yanayofanyika sasa hivi kwa mikoa ya Tabora na Kigoma yalitakiwa yafanyike 30 years back)
 

"ukawa @ work"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…