Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,757
- 21,986
Ndugu wana jamii forum Nawasalimu kwa jina la Mnyezi Mungu Muumba wetu.
Naleta maada hii kwenu ili kuwaeleza maswahibu yanayoniandama moyoni mwangu ili kama kuna yeyote aliyepitia basi tupeane faraja.
Mimi ni kijana wa kiume ambapo tarehe 30/12 mwaka huu ntatimiza umri wa miaka 26, nikiwa kidato cha sita mwaka 2012 nilipoteza baba na mama walipopata ajali na kufariki, kumbuka Mimi ndio kijana pekee wa kiume na Dada yangu mkubwa tu, nilijikaza kiume ambapo mwaka 2013 februari nlihitimu kidato cha sita, Nilijiunga na mafunzo ya JKT pale Ruvu JKT, bahati nzuri nlikuwa moja ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kwenye shabaha na kuahidiwa kuingizwa JWTZ iwapo tungependa.
Nilishauriwa na ndugu na jamaa kuendelea na elimu ya chuo kikuu ili hata kama nataka kujiunga JW niwe na shahada tayari, nliamua kusoma degree ambapo 2016 julai nlihitimu elimu ya chuo kikuu, nlipata shule ya kufundisha ya private,
Miezi michache baadae nlikutana na kaka yangu wa ukoo ambaye ni moja ya viongozi wakubwa katika awamu hii ( sitaji jina) aliniomba niache kufundisha ili nikasimamie mradi wake huku akiahidi kunilipa mshahara kila mwezi. nilikubaliana nae....nlianza kazi vizuri katika huo mradi miezi kadhaa ikapita hata kupewa mshahara wangu kitu kilichopelekea Mimi kuanza kuuza mpunga nlionunua huko morogoro kwa mama mdogo ili nijikimu kimatunizi na mambo mengine.
Baada ya mda Mimi na Dada yangu tuliamua kugawana pesa ambayo iliachwa na wazazi wetu, nlipata kama milioni tatu hivi ( 3,000,000/=). Nlinunua kiwanja na kufungua biashara ya Grocery ambayo ilikuwa ikinilipa vizuri tu, mda huo nliendelea kufanya kazi kwenye kampuni ya huyu kaka angu japo nlizidi kuwa na malimbikizo ya mshahara wangu maana sikuwa nikilipwa kila mwezi.
Sikujali hilo na nikapata Dada mmoja ambaye baadae nikaamua kumuoa japo bado hatujafunga ndoa rasmi lakini nlishajitambulisha kwa wazazi na nduguze mambo yakawa sawa,
Zengwe limekuja hivi karibuni ambapo biashara ya hiyo grocery ilianza kudorola na kujikuta mambo yangu hayapo sawa kabisa,
Pia nimeundiwa zengwe la kuwa Nina loss kwenye biashara ya jamaa ambapo malimbikizo yangu tangu nianze kufanya kazi yanafikia milioni tatu hivi!!! niliamua kuchukua mkopo ili nifufue grocery yangu ambayo ndio inanipa ridhiki ya kila siku,
Ninaumia sana jamani hasa nikikumbuka kuwa nilipata ajira ya kufundish nikaiacha kwa kulaghaiwa na mtu mkubwa wa karibu ninayemuamini sana.
Mpaka inafika mda nawaza bora nisingeoa huyu binti wa watu ili nisimuweke kwenye hali ngumu kama hii maana naelekea kudhulumiwa haki yangu huku hali yangu mbaya kiuchumi,
imefikia hatua nataka niuze pikipiki yangu ili nijaribu bahati zingine. maana sina namna sasa.
Naombeni ushauri nifanyeje ili nipate haki yangu toka kwa huyu (kigogo) kaka yangu.
NB: naomba ushauri jamani na uzoefu wenu.