Hii maana yake zoezi la kusajili laini limekuwa gumu

Hii maana yake zoezi la kusajili laini limekuwa gumu

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Milioni 19 ndizo namba zilizosajiliwa, milioni 29 bado kusajiliwa. Kikwazo kikubwa ni kitambulisho cha taifa. Kwa nini sasa kisitumike kitambulisho cha kupigia kura kama suala ni fingerprint? Au kuna sababu ingine kwamba kila Mwananchi awe na kitambulisho cha taifa?

Kama kweli zitafungwa laini hizo 29 milioni maana yake, kampuni hizi za simu zinaenda kupata mtikisiko mkubwa kimapato, na zitakwama pa kubwa.
Screenshot_20191207-075857~2.jpeg
 
Hawa jamaa sijui wana akili gani.. Id hawataki kutoa then wanakazana watafunga line.
Kwahiyo lengo lao hasa ni lipi?
Nadhani wangehakikisha kila mtu kapata id ndo waje na hizo ngonjera zao!
 
Hii nchi yetu wazee wa dedline, wanasubiri ile siku ya misho, then tunajua siku zitaongezwa..... 😁😁😁
 
Hii nchi yetu wazee wa dedline, wanasubiri ile siku ya misho, then tunajua siku zitaongezwa..... [emoji16][emoji16][emoji16]
Suala si deadline, suala ni changamoto ya kitambulisho.
 
Waziri alishasema hamna laini zitakazofungwa

nilipandisha uzi MODS wakauminyia kwenye library yao.
 
mimi wamenitumia namba ya kitambulisho. Nishasajili. Nilikwenda nida bagamoyo tarehe 12 mwezi wa 9.
 
Milioni 19 ndizo namba zilizosajiliwa, milioni 29 bado kusajiliwa. Kikwazo kikubwa ni kitambulisho cha taifa. Kwa nini sasa kisitumike kitambulisho cha kupigia kura kama suala ni fingerprint? Au kuna sababu ingine kwamba kila Mwananchi awe na kitambulisho cha taifa?

Kama kweli zitafungwa laini hizo 29 milioni maana yake, kampuni hizi za simu zinaenda kupata mtikisiko mkubwa kimapato, na zitakwama pa kubwa.View attachment 1284387
Mkuu kampuni za simu hazitaweza kuyumba kabisa! Pesa waliyokwisha waibia wateja wao ni nyingi sana kiasi cha kuweza kuwasustain kwa miaka 20 mbele
 
NIDA ni ........ Namba zetu za cm wanazo kwani tuliholozesha ktk form za maombi ya kitambulisho, watume tu Namber zetu.

Watume tuu.
 
Nasbiri wanifungie ndo nikasajili wanifungulie.
Hapo wasumbuke kidogo sio kula mishahara ya bure.
 
Hii nchi sijui ni uzembe au nini, wanashindwaje kurahisisha kazi kwa ku-link databases za mitandao ya simu na nida tena bila kusumbua wateja?
 
*BREAKING NEWS KUTOKA NIDA*

Ikiwa zimebaki siku 23 tu line zote ambazo hazijakamilisha usajili kufungiwa, NIDA wamezindua njia mpya ya kupata namba ya kitambulisho bure na haraka zaidi

Hakuna tena haja ya kudownload app wala kupoteza muda kwenye foleni

Bonyeza hapa kupata namba yako sasa: KITAMBULISHO - ShortUrl - Make your links short & powerful!

*TAFADHARI SHARE IWAFIKIE WENYE UHITAJI, SIKU ZIMEBAKI CHACHE SANA*
 
Back
Top Bottom