Hii logic imekaaje kuhusu siku sahihi ya ibada?

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,550
Wakristo wengi uabudu jumapili kama siku ya ibada.

Wakristo wengi uaminishwa kuwa Wayahudi ni watu wateule wa Mungu. Taifa la Mungu

Wayahudi ufanya ibada siku ya Jumamosi.

Kwanini wakristo hawaabudu Jmosi kama Wafanyavyo Wayahudi?

Na ukienda makanisa mengi unakuta hadi bendera za Israel zimepandishwa!

Naitaji majibu yenye logic tu...wafia dini siwataki hapa!
 
Wakristo ni wafuasi wa Yesu.Luka 4:16(Akaenda Nazareti pale alipolelewa na Siku ya Sabato akaingia kwenye Sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake......)Nadhani umepata jibu,Mungu na akutangulie na wote wasomao.
 
Wayahudi ni wa kale, wanasimamia agano la kale, Wakristo ni wa Yesu Kristo. Yesu Kristo alikuja duniani na kukuta wayahudi na sheria zao za kuabudu jumamosi yani muendelezo wa ya kale,

Yesu Kristo yeye akatengua ya kale yakawa mapya, likazaliwa agano jipya chini ya muongozo na sheria za Yesu Kristo na sio za uyahudi.

Wakristo wanafata ya Yesu hawafati ya wayahudi maana myahudi ni binadamu kama binadamu mwingine na ndie aliyemsulubisha Yesu na mpaka leo hii kuna wayahudi wanaamini Yesu hakuwahi kuja bado wanamsubiri.
 
Soma Luka 4:16 Desturi ya Yesu ilikuwa nini?
 
inategemeana na imani yako. kwangu mimi, siku sahihi ya ibada ni kila siku, tumeumbwa tumwabudu Mungu kila siku. ila kwa wengine ni jumamosi, wengine ijumaa, wengine jumapili n.k. ndo maana nasema inategemeana na imani yako.
 
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Wakolosai 2:16
 
Wayahudi ni wa kale, wanasimamia agano la kale, Wakristo ni wa Yesu Kristo. Yesu Kristo alikuja duniani na kukuta wayahudi na sheria zao za kuabudu jumamosi yani muendelezo wa ya kale,

Yesu Kristo yeye akatengua ya kale yakawa mapya, likazaliwa agano jipya chini ya muongozo na sheria za Yesu Kristo na sio za uyahudi.

Wakristo wanafata ya Yesu hawafati ya wayahudi maana myahudi ni binadamu kama binadamu mwingine na ndie aliyemsulubisha Yesu na mpaka leo hii kuna wayahudi wanaamini Yesu hakuwahi kuja bado wanamsubiri.
Yesu alitengua na Sabato?!
 
Hivi si Yesu alisema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza..na kuna mahali alisema yeye ni bwana wa sabato..na pia alisema amekuja kitimiza maagizo ya Baba..

Halafu kwani wayahudi waliamini Mungu yupi na Yesu alitumwa na Mungu yupi?

#MaendeleoHayanaChama
 
Yahsua (Yesu) alisali jumamosi (sabato) kama wafuasi wa agano la kale, kwa hiyo hakubadili siku ya kusali ka wasemavo wengine. Wakristo na wayahudi siku ya kusali ni ile ile (sabato - jumamosi).

Jumapili iliingizwa na warumi baada ya kuanzisha kanisa mama katoliki kwa sababu za kibinadamu ikawa na mshiko. Hatimaye miaka ya mbeleni, kina Luther wakapingana na kanisa mama kuhusu mengi mojawapo siku ya kusali - wakajitenga. Ambacho nipo gizani ni jinsi gani makanisa ya kina Luther yalirudi kusali jumapili.

Swala la wateule wa Mungu limeandikwa ndani ya biblia... swala la upeperushaji wa bendera ya israeli ni la sababu ya elimu bubu kwa sababu wakazi wa kule leo hii ni wayahudi feki
 
Tofauti ya wakristo na wayahudi ni moja tu -
wayahudi - Yahsua (Yesu) sio mesaya alotabiriwa na kuandikwa na agano la kale, wakamkataa, bado wanamsubiria
wakristo - Yahsua ndo mesaya alotabiriwa na kuandikwa...

zaidi ya hapo, Yahsua hakubadili mila na desturi za ukristo wa agano la kale wala kuashiria na kuruhusu sheria zibadilike - mfano ulaji wa kitimoto, siku ya kusali, nk
 
Ninachoamini mimi kwamba unasali siku gani haitakuwa kigezo cha hukumu yako
Sali siku yoyote cha msingi penda wengine baasi mbingu unaingia mapema sana.
 
Wayahudi ni wa kale, wanasimamia agano la kale, Wakristo ni wa Yesu Kristo. Yesu Kristo alikuja duniani na kukuta wayahudi na sheria zao za kuabudu jumamosi yani muendelezo wa ya kale,

Yesu Kristo yeye akatengua ya kale yakawa mapya, likazaliwa agano jipya chini ya muongozo na sheria za Yesu Kristo na sio za uyahudi.

Wakristo wanafata ya Yesu hawafati ya wayahudi maana myahudi ni binadamu kama binadamu mwingine na ndie aliyemsulubisha Yesu na mpaka leo hii kuna wayahudi wanaamini Yesu hakuwahi kuja bado wanamsubiri.

Yesu mi Myahudi
Dini yake Myahudi
Mungu wake Yahwe
Siku ya kuabudu Jumamosi/Sabato siku ya Saba ya Juma Kwa Kalenda ya kiyahudi.
Alizikwa Kiyahudi.
Siku zote alizosherekea ni zakiyahudi.
Jina lake la kiyahudi
Mama yake ni Myahudi
Akachukua ukoo wa Yusuph myahudi.

Alikufa siku ya ijumaa(siku ya sita Kwa mujibu wa Kalenda ya kiyahudi)

Pia atakuja siku ya Ijumaa ambayo ndio inatarajiwa kuwa siku ya Kiama.

Wanaoabudu siku ya jumapili wanafuata mfumo wa Dini za Ulaya hasa taifa la kirumi.

Hata hivyo siku zote ni siku za Ibada. Kwa sababu maisha ya mwanadamu ni ibada.
Ila siku ya sabato ni siku ya Mungu aliyoiteua ili viumbe binadamu wamtukuze siku hiyo Kwa mujibu wa dini ya kiyahudi.

Quran nayo inathibitisha Hilo, Quran unamtambua siku ya Sabato ni jumamosi na sio jumapili.

Huo ni muhtasari
 
Ninachoamini mimi kwamba unasali siku gani haitakuwa kigezo cha hukumu yako
Sali siku yoyote cha msingi penda wengine baasi mbingu unaingia mapema sana.

Kuingia mbinguni Inategemea na Uelewa wa Mtu.

Kama ulikuwa unajua kabisa kuna amri kuhusu siku ya Ibada iliyowekwa wakfu ukapuuzia Kwa kudhani ni amri nyepesi basi litakuwa ni kosa la uasi.
Labda uwe ulikuwa hujui na hukuwa na mazingira ya kujua.
 
Waayhhuudii waliabudu Mara moja TU kwa mwaka

Unazijua sikukuu za Wayahudi Mkuu?

Kwa kukusaidia Kwa uchache!

1. Kila siku ya sabato ni sikukuu ya Wayahudi. Kila wiki.

2. Mwezi wa Saba wa kiyahudi ni sikukuu

3. Mwaka wa Saba wa kiyahudi ni sikukuu ambayo watapaswa wapumzike na wafurahie na kumtukuza Mungu.

4. Sikukuu ya vibanda

Miongoni mwa sikukuu zingine Kwa mujibu wa dini ya kiyahudi
 
Wayahudi ni wa kale, wanasimamia agano la kale, Wakristo ni wa Yesu Kristo. Yesu Kristo alikuja duniani na kukuta wayahudi na sheria zao za kuabudu jumamosi yani muendelezo wa ya kale,

Yesu Kristo yeye akatengua ya kale yakawa mapya, likazaliwa agano jipya chini ya muongozo na sheria za Yesu Kristo na sio za uyahudi.

Wakristo wanafata ya Yesu hawafati ya wayahudi maana myahudi ni binadamu kama binadamu mwingine na ndie aliyemsulubisha Yesu na mpaka leo hii kuna wayahudi wanaamini Yesu hakuwahi kuja bado wanamsubiri.
Nioneshe kwenye Biblia Yesu aliposali jumapili.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Kama yote hayo mnayajua mnayafata
Tenda mema ishi maisha mema..utaenda mbinguni bure kabisa
 
Back
Top Bottom