Hii la mahakama ya kadhi limekaaje?

Hii la mahakama ya kadhi limekaaje?

Status
Not open for further replies.
Hili la mahakama ya kadhi limekaaje mbona tulihamasishana sana lakini kwenye rasimu ya katiba limekwepwa

haya ni kati ya mambo magumu ambayo tuliambiwa hayajadiliki pamoja na like la OIC.
 
Huo ndiyo uhuni wa ccm,kwenye kampeniya urais walituahidi litashughulikiwa lakini wametuona sisi kama watu wasio na akili,wametufanya ngazi ya kufanikiwa malengo yao ya kisiasa.
Hapo sasa inabidi tubadilike habari ya kutumiwa kama ngazi na wanasiasa kwa malengo ya vyama vyao sasa iwe mwisho.
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!
 
Mmh! Ngumu kumeza

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Waislamu walishiriki katika kutoa maoni kuhusu kurejeshwa Mahakama ya Kadhi lakini hakuna aliyetegemea kuwa Warioba atatupa Mahakama ya Kadhi!

Ninachotaka kusema ni kuwa hakuna jipya! ilitegemewa na Waislamu kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litatupwa, lakini kama wasemavyo wazungu There is always plan B.
 
mambo yote yanafanyka kama ALLAH alivyo kadiria mahakama ya kadhi muda wake ukifka tuta ipata tu. assalam alykum
 
Huo ndiyo uhuni wa ccm,kwenye kampeniya urais walituahidi litashughulikiwa lakini wametuona sisi kama watu wasio na akili,wametufanya ngazi ya kufanikiwa malengo yao ya kisiasa.
Hapo sasa inabidi tubadilike habari ya kutumiwa kama ngazi na wanasiasa kwa malengo ya vyama vyao sasa iwe mwisho.
Haahaaa - habari ndio hiyo!
 
hili la mahakama ya ardhi mlilipigia kelele na nani! mlishambiwa ruksa kulianzisha but lisitegemee mkono wa serikali, coz ni mambo ya kiislamu hayo!
 
Wameliacha kwa nchi husika lijadili,zanziba na bara walijadili na kuliamua kama nchi huru!
Naona wachangia mada hawajasoma vizuri hotuba ndio maana wanakurupuka. Tume imetoa rasimu kwa vitu vya Muungano,
swala la mahakama ya kadhi si la muungano, hivyo imeliacha kwa nchi husika. Tukumbuke pia kuna swala la mikataba inayohusu raslimali za taifa hakulisema; napenda kujuzwa hilo litawekwaje kwa Tanzania bara?
 
Waislamu walishiriki katika kutoa maoni kuhusu kurejeshwa Mahakama ya Kadhi lakini hakuna aliyetegemea kuwa Warioba atatupa Mahakama ya Kadhi!

Ninachotaka kusema ni kuwa hakuna jipya! ilitegemewa na Waislamu kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litatupwa, lakini kama wasemavyo wazungu There is always plan B.

Kwa moyo mmoja serikali ya baba wa Taifa iliwasaidia kuwa na chombo chenu BAKWATA, matokeo yake anatusiwa hadi huko aliko...Simameni wenyewe kwa miguu yenu hamjakatazwa kuanzisha hiyo Mahakama yenu Mungu awape nini tena? Soma ibara ya 31 ya Rasimu....

Uhuru wa

imani ya dini

31.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,
imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa
ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya
taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya
kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na
wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za
nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru
wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote
itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni
mwa wananchi.
(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno
mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa
kwa maana hiyo.

Huo ndiyo uhuni wa ccm,kwenye kampeniya urais walituahidi litashughulikiwa lakini wametuona sisi kama watu wasio na akili,wametufanya ngazi ya kufanikiwa malengo yao ya kisiasa.Hapo sasa inabidi tubadilike habari ya kutumiwa kama ngazi na wanasiasa kwa malengo ya vyama vyao sasa iwe mwisho.
Kama mlitumiwa mkakubali hiyo ndo adhabu yake inawafaa sana, hata siku nyingine watakuja tena watawatapeli mtakubali tu hii ndo bongo bwana.
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!

Sasa hawa jamaa wanataka mambo ya chumbani yaamuliwe na wapita njia?
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!

hawajajifunza ya BAKWATA
 
Akitokea mwanasiasa mwingine akaahidi mahakama ya kadhi, jamaa watampigia kura tena!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom