Hii kitu inanikera sana

Joined
Sep 20, 2014
Posts
69
Reaction score
14
Mi binafsi hiki kitu sikipendi kabisa,

kitendo cha wazazi wa mwanamke kuwapa nyumba ama kiwanja kabla ya ndoa au siku ya ndoa kama zawadi...
mi hiki kitu sitaki kabisa kije nitokea maishani naona heri nianze kidogo kidogo hata kama ni kwa shida ila nijenge kwa nguvu zangu binafsi kama mke hana kipato ama pia tujenge wote kama kajaliwa kipato sababu vyovyote mali itakua yetu sote na watoto wetu hapo baadae.

Ila swala la kupewa hizo zawadi binafsi kama ni kabla ya ndoa naweza nikaahirisha ndoa maana mi fikra zangu na kwa jinsi nlivyoona ndoa za wengi unakuwa kama mwanamme umenunuliwa..

je hii perception niliyonayo ni sahihi kwel jaman maana pia huwa napenda kufaham vitu kupitia shauri mbalimbali

Je ni sawa kwel hii!! nini mtazamo wenu wadau
 

Sio umaskini unaokusumbua kweli
 
Ukipewa zawadi ya kuku mmoja wa kienyeji unanuna na ukipewa kiwanja hutaki we binadamu wa namna gani? KWELI HUMAN WANTS ARE UNLIMITED
 
Kipokee hicho kiwanja, sio lazima ukitumie kujenga. Zawadi haisusiwi mkuu.

Kinaweza kukufaa siku yoyote
 
Sijui hata nikuambiaje. Cha muhimu ni upate umiliki halali, kupewa Nyumba au Kiwanja sio zambi.
 
Hata ukipokea nyumba, umeambiwa lazima uishi humo??..

Unaweza ukaipangisha wakati mnajenga yenu..

My Take: unaweza kugeuza zawadi kama chanzo cha mapato. Kuzawadiwa nyumba au kiwanja, haimaanishi wewe ni masikini, bali ni upendo kwa wazazi kwenu.
 
Hata ukipokea nyumba, umeambiwa lazima uishi humo??..

Unaweza ukaipangisha wakati mnajenga yenu..

My Take: unaweza kugeuza zawadi kama chanzo cha mapato. Kuzawadiwa nyumba au kiwanja, haimaanishi wewe ni , bali ni upendo kwa wazazi kwenu.


sawa nakubaliana nanyi je nyumba kiwanja kidogo sio mbaya nyumba je?
 
Ukipewa zawadi ya kuku mmoja wa kienyeji unanuna na ukipewa kiwanja hutaki we binadamu wa namna gani? KWELI HUMAN WANTS ARE UNLIMITED


hapana dont generalize wengine zawadi ndogo wanaipokea bila manung'uniko
 
Hata ukipokea nyumba, umeambiwa lazima uishi humo??..

Unaweza ukaipangisha wakati mnajenga yenu..

My Take: unaweza kugeuza zawadi kama chanzo cha mapato. Kuzawadiwa nyumba au kiwanja, haimaanishi wewe ni , bali ni upendo kwa wazazi kwenu.

yap your thoughts are good ila unajua nina mfano halisi wa mtu mmoja alioa mwanamke mzaz wa mwanamke ni tajiri so akawakabidhi nyumba wameishi miaka kadhaa vizur gafla kampuni aliokua anafanya mume kaz ikafilisika sa hapo ndo manyanyaso yakaanza ooh mwanamme gan unantegemea mwanamke nyumba hujajenga n.k navokuambieni hivi sasa ndoa imevunjka...
mwanamke ana kazi bado ila mwanamme hana kaz had sasa

kwa hiyo bado nna mashaka sana na uamuz wa kupokea nyumba siwez kukata kama nmeshamuoa ila km sijamuoa nadhan ni sahihi nikikataa au kuhairisha ndoa aya manyanyaso yanaweza kukuua kwa mawazo
 
Apate wapi hata.hicho cha zawadii? Mtu mbinafsi utamjua tu na gubu juu.

siwapendi watu mnaopenda maugomvi sina haja ya kukutajia utajir wangu kuthibitisha sina hana na hicho kizawad by the way sijasema nimepewa zawadi ni mfano tu...
its just a possibility that can happen to anyone
ulisoma vizur kwel, ugomvi na chuk sio mzur utakufanya ufe kabla ya siku zako
 
Siyo kila mtu anapewa zawadi ya nyumba kwenye ndoa zao. Ukiona mpaka unapewa ujue una nyota. Kwa nini usichukue. Alafu unajua aliyekuwa nacho anaongezewa, asiyekuwa nacho ananyanganywa hata kile kidogo. Ukiona unapewa zawadi kama nyumba ujue na wewe pia unajiweza ile ni nyongeza tu.
 

Hahahaaaa uwiiii ni shedaaah eti ugomvi umajua maana ya ugomvi kiufupi wewe ni mbinafsi hakuna mzazi anayeweza kutoa zawadi bila kuhakikisha mwanawe yupo kwenye ndoa yenye baraka zote ya wazazi a kanisani au msikitini zaidi ya hapo tiendelee kupiga story.
 
ichukue nawe umzawadie mkeo.. halafu endelea na mipango mingine ya maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…