Hii kesi, kuna kifungo kina nyemelea hawa watu

Muda wa kumkubali Mbowe kwenye Jamii umeisha.

Kila kitu kina Expiring Date.
Mbowe ameexpire kana Rais wa Sudani, Gadaf, Mabuto na madikteta Wengine waliowahi kutokea duniani.
Hakuna mtu nanyekubalika muda wote.

Mbowe mambo mengi anayakosea kutokana na kuwaza sifa binafsi ,zaidi kuliko jamii .
Kuna watu wananiuma sana ninapowaza kuwa wanaweza wakafunga lakini sio Mbowe.
Mbowe anapaswa kufungwa kifungo cha Maisha mana amesbabisha Demokrasia ya nchi hii kutoweka. Ameshindwa kucheza na siasa za Awamu ya Tano badala yake akalazimisha kwenda na mambo ya awamu ya Nne .

Kuhamasisha maandamano ya Ghafla ni jambo la hatari sana na halikawahi kukubalika popote duniani.

Ni vema Aliyelazimisha maandamano akafungwa gerezani.
Haki itendeke.
Kwa hiyo mbowe ni dictator wa taifa gani?. Naomba nikumbushe, na ikiwezekana tuhamasishe maandamano tumutoe madarakani kama bashiri na wengine uliowataja.
 
yaani kati ya wote alimuona Mbowe tu
Sasa hapa ndio amemaliza huyu mwela?
Subiri kwenye Cross examination atavyoumbuka huyu mwela.

Yaani hata kama defense attorney ningekua mie I could grill his stupid evidence.
 
Hadithi za Mfalme Juha hizo...... Unataka kumaanisha kuwa Mkurugenzi amabaye ni Msimamizi wa uchaguzi ndio chanzo cha yote hayo? Maana bila yeye Chadema wasingeandamana Polisi wasingekuja Aqwilina Asingekufa. Vp mkurugenzi na yeye yupo Mahakami au?
Hoja hapa wameshitakiwa kwa kosa gani? na hakika si mauaji. Hayo mengine watajieleza kwa hakimu sio mimi. Maandamano yoyote lazima yawe yametolewa taarifa Polisi watamuonyesha hakimu kibali chao.
 
Wametelekeza vijana wengi magerezani,kwa ujumla Mbowe ni dj haswa,hahaha!

Hata Elibashiri aliweka watu wengi ndani waliokuwa wanampinga. Leo yuko nao ndani kwenye gereza hilo hilo alilowapeleka. Kwa hii mahakama ambayo jaji mkuu anashinda ikulu tayari jiwe ameshamuandikia hukumu iweje. Hivyo hakuna atakayeshangaa hukumu hiyo. Sasa hivi mahakama ya Afrika mashariki ndio iko huru, sio hizo mahakama za wasaka madaraka
 
Kumbe waandamanaji walikimbia? sasa kina mbowe kosa lao ni kukimbia au vipi? dah hii nchi hii...!!!
 
Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Gerald Ngiichi ameieleza mahakama hiyo kuwa aliamuru askari kupiga risasi hewani kwa ajili ya kutawanya maandamano ya viongozi na wafuasi CHADEMA.
Ushahidi huo ambao wa kwanza kutolewa katika kesi hiyo, SSP Ngiichi alidai kuwa aliamuru risasi zipigwe kwa sababu njia ya kutumia mabomu ya Moshi ‘Machozi’ ilishindikana kuwatanya.
"Nililazimika kutumia njia ya mwisho ya kutumia silaha za moto kupigwa hewani kutoka na waandamanaji kutotii ilani tatu nilizozitoa katika umati huo wa waandamanaji kwa kutumia kingo'ra nikiwa katika gari la polisi," alidai Ngichi.
Alidai kabla ya kutumia njia ya mwisho ya kuamuru askari wake wa vikosi vya doria kupiga risasi juu, aliamuru kikosi cha askari walikiwapo katika eneo hilo kupiga mabomu ya moshi kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wanaongozwa na viongozi wa chama hicho.
Alidai wakati askari wake wakiendelea kurusha mabomu ya moshi kwa waandamanaji hao, hawakufanikiwa vizuri kutokana na moshi wa mabomu hayo kuelekea upande walipo askari hao
.
"Zoezi la kupiga mabomu waandamanaji hao lilikuwa hafifu kutokana na moshi kuelekea upande walipo askari badala ya kwenda kwa waandamanaji kutokana na upepo uliokuwapo eneo hilo hali iliyopelekea waandamanaji kutosambaratika" alidai Ngichi.
Alidai katika harakati za kurusha mabomu kwa waandamanaji hao, askari polisi wawili ambao ni PC Fikiri na Koplo Rahim waliokuwapo eneo la tukio walijeruhiwa kwa mawe na kuanguka chini.
"Baada ya kuanguka chini askari hao niliamuru askari wengine watoe msaada kwa majeruhi hao kwa kuwaondoa katika eneo hilo na niliamuru kikosi cha mabomu kirudi nyuma na kikosi cha risasi kisonge mbele ili kukabiliana na waandamanaji hao," alidai.
Alidai askari wenye silaha walisogea mbele na kupiga risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokiwa wanataka kuchukua silaha baada ya askari wake wawili kujeruhiwa na kuanguka chini.
"Risasi zilivyopigwa hewani kishindo kilikiwa kikubwa hali iliyopelekea watu wengi kukimbia akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, sikujua kama mheshimiwa Mbowe anajua kukimbia namna hiyo," alidai Ngichi
Pia amedai, baada ya waandamanaji kusambaratika, alifanya tathmini na kubaini kuna majeruhi wawili ambapo alikuwepo Akwilina aliyewahishwa Hospitali ya Mwananyamala na baadae kuripotiwa kuwa amefariki.
Ngiichi ambaye ni Ofisa Operesheni wa Kipolisi Kinondoni, na shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13, 14 na 15, 2019 kwa ya kuendelea kusikilizwa.
Kamanda kajikanganya na ushahidi wa uongo, alifanya tathmini na kugundua watu watatu wamejeruhiwa akiwemo Akwilina! Akwilina alipigwa risasi ndani ya basi ilikuwaje akaokotwa chini, mbona kondakta wa basi ambaye pia alijeruhiwa hajamtaja! Hayo mabomu hayakuwafikia waandamanaji! Na moshi mkubwa kiasi cha kutokuona ulitoka wapi, labda kama mabomu hayo ni ya kisasa.
 
"Risasi zilivyopigwa hewani kishindo kilikiwa kikubwa hali iliyopelekea watu wengi kukimbia akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, sikujua kama mheshimiwa Mbowe anajua kukimbia namna hiyo," alidai Ngichi"
Alidai wakati askari wake wakiendelea kurusha mabomu ya moshi kwa waandamanaji hao, hawakufanikiwa vizuri kutokana na moshi wa mabomu hayo kuelekea upande walipo askari hao
.
"Zoezi la kupiga mabomu waandamanaji hao lilikuwa hafifu kutokana na moshi kuelekea upande walipo askari badala ya kwenda kwa waandamanaji kutokana na upepo uliokuwapo eneo hilo hali iliyopelekea waandamanaji kutosambaratika" alidai Ngichi.
 
Kamanda kajikanganya na ushahidi wa uongo, alifanya tathmini na kugundua watu watatu wamejeruhiwa akiwemo Akwilina! Akwilina alipigwa risasi ndani ya basi ilikuwaje akaokotwa chini, mbona kondakta wa basi ambaye pia alijeruhiwa hajamtaja! Hayo mabomu hayakuwafikia waandamanaji! Na moshi mkubwa kiasi cha kutokuona ulitoka wapi, labda kama mabomu hayo ni ya kisasa.
si alisema aliamuru risasi zipigwe juu imekuwaje ikadaiveti hiyo risasi na kuelekea ndani ya DALDALA na kumresti in PISI AKWILINA wetu?
 
Back
Top Bottom