Hii kauli wadau mmeichukuliaje?

Hii kauli wadau mmeichukuliaje?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,200
Reaction score
162,758
Just a summary:

Raisi anapowaambia wasadizi wake kuwa wenye wajubu ni yeye kama raisi na makamu wake ambao ndio walizunguka nchi nzima na amewataka wasaidize wake waache kusumbua wananchi kwani kawateua tu na wengine hata hawakutarajia na kwamba hawana political responsibility.

kawaambia pia kabla hawajaamua jambo lolote wamuone yeye na makamu wake kwanza kupata idhini yao.

Mh.anasisitiza kiongozi yoyote asieweza kufuata maagizo aache kazi.
 
Raisi anapowaambia wasadizi wake kuwa wenye serikali ni yeye kama raisi na makamu wake na kwamba wao ndio walizunguka nchi nzima na pale alipoongeza kwa kuwaambia wasaidize wake waache kusumbua raia kwani kawateua tu na wengine hata hawakutarajia na kwamba hawana political responsibility na kabla hawajaamua jambo lolote wawaone yeye na makamu wake kwanza.
Mkuu umebananishwa nini ? "Kunywa maji mwanangu" halafu rudia kuandika

One man show mpaka kieleweke hakuna cha bunge mahakama wala watuele wake

Oh tumeipenda mwaka huu tumejipangaa
 
Raisi anapowaambia wasadizi wake kuwa wenye serikali ni yeye kama raisi na makamu wake na kwamba wao ndio walizunguka nchi nzima na pale alipoongeza kwa kuwaambia wasaidize wake waache kusumbua raia kwani kawateua tu na wengine hata hawakutarajia na kwamba hawana political responsibility na kabla hawajaamua jambo lolote wawaone yeye na makamu wake kwanza.

Hivyo ndivyo mwnamume atakiwa kunguruma. Short & clear kama utashindwa kuhimili sepa, we ulikua bafuni kutoka unasikia umekua mkuu wa mkoa au mkurugenzi usilete tabu kwa raia.
 
Dah! kwani Makonda alivyokuwa anadhalilisha watumishi wauma na kuwaita "vichaa" huku akijifananisha na Mungu ni nani aliyekuwa wa kwanza kumpongeza. Mkuu asicheze na akili za watu. Leo wanaowafukuza wamachinga wanaonekana ni waovu kuliko wanaodhalilisha watumishi wauma? Hii siasa ya ajabu sana; huku ni kuchanganya wananchi tu au kuuma na kupuliza mithili ya panya. Mkuu asipunguze moto; aendelee hivo hivo na wateule wake waendelee kuyatoa matamko dhalili; waendelee kufukuza wamachinga na kunyanyasa akina mama ntilie. hiyo ndo style ya kukurupuka na muasisi wa style hiyo anajulikana
 
Lakini kwa hili damu nzito kuliko maji, machinga wamefukuzwa sehemu nyingi hapa nchini na wamevunjiwa na kuporwa vitu vyao sikusikia akikemea, lakini tukio kutokea tu huko mbiyo kutoa tamko Kali, nashauri asiwe mkanda hata wale wa mtwara nao ni mama ntilie na machinga asisubiri hadi wa huko ndo atoe makaripio.
 
Kuna watu wajinga sana hapa nchini...

Serikali haifanyi kazi kwa kuangalia tukio moja pekee, ni hadi kuwepo na matukio zaidi ya moja ndipo inanyanyuka kukemea...

Kwa mfano, huwezi kumfukuza RPC au IGP kwa kuangalia tukio moja la ujambazi mkoani kwako au nchini, ni hadi kuwepo na utitiri wa matukio hayo ndipo uchukue hatua stahiki na mara moja..

Na ndo maana Rais aliona matukio zaidi ya wamachinga kunyanyasa yanaendelea ndo leo katoa tako la kukemea.
 
Umejiuliza mbona wale vijana wa UDOM walitimuliwa bila huruma?

Nachokiana hapa huenda mkuu ameshaanza kuona dalili ya yeye kuchukiwa na wananchi.
 
Kuna watu wajinga sana hapa nchini...

Serikali haifanyi kazi kwa kuangalia tukio moja pekee, ni hadi kuwepo na matukio zaidi ya moja ndipo inanyanyuka kukemea...

Kwa mfano, huwezi kumfukuza RPC au IGP kwa kuangalia tukio moja la ujambazi mkoani kwako au nchini, ni hadi kuwepo na utitiri wa matukio hayo ndipo uchukue hatua stahiki na mara moja..

Na ndo maana Rais aliona matukio zaidi ya wamachinga kunyanyasa yanaendelea ndo leo katoa tako la kukemea.
ha ha kwa sababu ni Mwanza Mbeya Arusha Dar es salaam hakumhusu ni mbaguzi mkabila sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom