Nimesikiliza interview ya Generali Kagame akiongelea jinsi anavoliona tatizo la huko Congo Mashariki.
Kiufupi anasema bila kumung'unya maneno kuwa wasipopatana anajitayarisha kwa vita na kwa olote litakalo jitokeza.
Tunakumbuka aisema hivyo kuwa atamshughulikia Kikwete mnamo miaka ya nyuma, na yaliyotokea baadaye baada ya jeshiusu lake la M23 kushughulikiwa kikamilifu huko Goma, ikabidi ajifungie ndani.
Sasa nauliza hiki kidomodomo cha kuichezea Congo kinatoka wapi?
Au kuna Taifa nyuma yake linalo mpa Jeuri Generali Kagame?