Hii iwe next move ya Chadema .... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii iwe next move ya Chadema ....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamayu, Nov 19, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Baada ya jana kutoka kwenye Bunge wakati JK alipotaka kuanza kutoa hotuba yake ya kuzindua Bunge, next move iwe kama ifuatavyo:

  1. Wabunge wa Chadema bila kuathiri kanuni za Bunge wasiwe viongozi au wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge - wawaachie akina Vicky Kamata, Rostam na wengine wa CCM, Hamad Rashid na wenzie wa CUF, Augustino Mrema wa TLP, Cheyo wa UDP na Kafulila, Mkosamali wa NCCR - Mageuzi;

  2. Serikali kivuli itakayoundwa na Chadema kila inapopewa muda wa kuongea Bungeni iwe imelenga kutekeleza ilani ya Chadema. Yaani debate itakuwa na proposers (JK's government) na opposers (Chadema's gov't i.e. shadow one). Na mara CCM wanapofanya utekelezaji wa shadow gov't ideas basi press conference ifanyike kuwafahamisha watanzania - kwa kifupi never reach a consensus [shadow government should be run as if it is a government in power];

  3. kama ilivyofanyika 'operation sangara', mgombea Urais kuomba wadhamini ndivyo hivyo lifanyike zoezi la kukusanya maoni ya wananchi wanaotaka mabadiliko ya katiba hasa yahusuyo uchaguzi mkuu [petition] ambayo itakabidhiwa kwa Mbunge wa Chadema na kuiwasilisha bungeni kama kanuni namba 34 ya Bunge inavyosema: na hili lifanyike mapema zaidi na kuhakikisha wapiga kura wa Njombe, Katavi na Msoga wanapewa nafasi ya ku-petition;
   
Loading...