Hii interview ilinifanya nicheke!

Hii interview ilinifanya nicheke!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Jamaa alikua na ndugu yake ndani ya taasisi,

Walihitajika watu 5 kwa kazi, shortlist ilikua na watu 130. Aliitwa na ndugu yake kama kuzuga tu wengine wasigundue siri.

Alipoingia chumba cha interview mswali yake yalikua hivi; Mombo vipi? Nyumbani hawajambo?Umekuja huku lini?Mzee hajambo? mwisho akaambiwa wasalimie home na tutakujulisha siku ya kuanza kazi.

Kwa sasa jamaa yuko kazini,

Uliza wengine maswali waliyokumbana nayo kwenye interview! Utachoka.
 
Mtoa mada, hivi umesoma vizuri kweli kwenye hiyo orodha ya majukwaa na kujua hili jukwaa gani!??
 
Ina maana hakukuwa na jopo la wasaili bali ndugu yake pekee ndiye aliyekuwepo na kumuuliza maswali hayo?

Anakuambia alikuwepo mtendaji mkuu na wakuu wachache wa idara.Alipoingia ndani ya chumba alikuta wote interviewer wote walikua na sauti moja kwa maana kua walishawaandaa watu wao.
 
Mtoa mada, hivi umesoma vizuri kweli kwenye hiyo orodha ya majukwaa na kujua hili jukwaa gani!??

Bwana ngonyani hili ni jukwaa lihusulo mambo ya kazi,Kama hujawahi kutana kitu kama hichi utabaki kusimuliwa tu, Kama unahisi ni simulizi tu na sio uhalisia basi huenda hujui kwamba kuna wahanga wa haya.Hii stori alikua anaitoa mtu aliepitia njia za mkato kuajiriwa kuliko wengine.Iliniuma sana ndo maananikasema tushirkishane kukea mambo kama haya
 
Sitaamini, kila nikiwaza panel yote waunge mkono kwa maswali ya kipuuzi namna hiyo.
 
hahahaa inawezekana mm nlienda interview mtu hata hajui anafanya interview ya nn.kaja anauliza kwan ni position gani?hata vyet na barua hakutuma.copy ya vyet imetolrwa hapo hapo barua imeandikwa hapohapo.kila kitu kasaidiwa na mmoja wa wasaili na wasaili walikuwa watano.mwngne kaja saa nane mchana wengne tuliambiwa interview itaanza saa mbili asubuh tukakaa had usiku.hao wawili hapo nimewafuatilia tayar wapo kazin yaan wamrajiliwa.
 
Anakuambia alikuwepo mtendaji mkuu na wakuu wachache wa idara.Alipoingia ndani ya chumba alikuta wote interviewer wote walikua na sauti moja kwa maana kua walishawaandaa watu wao.

Nimekubali, hakuna kisichowezekana nji hii.
 
hahahaa inawezekana mm nlienda interview mtu hata hajui anafanya interview ya nn.kaja anauliza kwan ni position gani?hata vyet na barua hakutuma.copy ya vyet imetolrwa hapo hapo barua imeandikwa hapohapo.kila kitu kasaidiwa na mmoja wa wasaili na wasaili walikuwa watano.mwngne kaja saa nane mchana wengne tuliambiwa interview itaanza saa mbili asubuh tukakaa had usiku.hao wawili hapo nimewafuatilia tayar wapo kazin yaan wamrajiliwa.

Sasa ndicho nilichosimuliwa kinafanana hiki,Kuna watu hawaami mambo kama haya na pengine hayajawahi kuwakuta!Ndio wanaolia kila siku kwa mambo ya undugu kazini, matokeo yake unalalamika tu na kuzunguka na vyeti vyako kutwa nzima bila mafanikio.Sisi tulikwishaona na tunawaambia mnapoapply mjue kuna haya.
 
mimi uliposimulia tu nimeamin
 
Hamjui kuwa membe na kikwete ni mtu na ndugu yake,

Baba mmoja ila mama tofauti
 
Hayo maswali aliyoulizwa ni ya msingi kwenye interview lakini kwamba ndio yalikuwa maswali pekee ni uongo !!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom