Hii inaweza kuwa imesabishwa na nini?

Kibada

Senior Member
Apr 5, 2012
123
17
Jamani yamenikuta hiyo juzi! Nilikula nyama ya mbuzi kwenye bar moja hivi mimi na rafiki yangu.. Baada kama ya nusu saa hivi nikaanza kuwashwa mwilini sana... Mpaka leo ndio imepungua... Nikamuuliza rafiki yangu nae kasema aliwashwa kama mimi...! Hii inaweza kuwa imesababishwa na nini?
 
Pole sana mkuu, ngoja waje wataalam, lakini lazima tuwe na tahadhari sana na hizi nyama maana siku hizi uchakachuaji umekithiri sana.Mtu sababu ya tamaa ya pesa anaweza kuuza nyama ya nani hii huku akisema ni ya mbuzi.
 
Unaweza kuwa mlikula nyama ya MBWA,
Mnaweza kuwa hiyo nyama ilitengenezwa kwa mafuta ya jenereta,
Ushauri: Nenda kwa daktari ukapime upate kujua tatizo
 
sio utani kaka! na uhakika hiyo ilkuwa ni nyama ya Kondoo maana hata mimi ilwahi kunikuta na baadaye nikaja kubaini kuwa ilikuwa kondoo na sio mbuzi!
 
Mkuu nimecheka sana,utasababisha jamaa akose amani kabisa
 
ulikuwa wapi;?, dar najua mbuzi kwenye bar ni uchafu tu. mbuzi mikoani fresh from village anatiwa kisu analiwa na kichuri chake sasa kama ni bongo hapo lazima ni kaumbwa kadogo tu.
 
Nilielezwa na mtu mwingine pia kwamba anaweza kuwa ni kondoo..
 
Mkuu nimecheka sana,utasababisha jamaa akose amani kabisa
Nilipoona hii comment kwanza nikaingia mtini... Nilitapika usiku nilikuwa nafikiria labda nilikula nyama ya MBWA... Nilienda kwa daktari nilapewa vidonge vinaitwa celestimine kama sikosei.. Nilikunywa kimoja tuu kuwashwa kukapungua... Nimepona sasa lakini bado nina makovu ya kujikuna..
 
ulikuwa wapi;?, dar najua mbuzi kwenye bar ni uchafu tu. mbuzi mikoani fresh from village anatiwa kisu analiwa na kichuri chake sasa kama ni bongo hapo lazima ni kaumbwa kadogo tu.

Kiongozi nimekoma kula bar... Nitakuwa nagonga vinywaji tu... Lakini mwenzangu mpaka leo anawashwa juzi alikwenda Aga Khan lakini hali yake sio nzuri... Alitumia dawa nilizopewa mimi lakini hola!
 
Huwa una kawaida ya kula mbuzi? Inawezekana ukawa na allergy tu. Pia inawezekana kuwa mafuta yaliyopikia yakawa na reaction kwako (japo sidhani kama ni coincidence kwenu wote wawili itokee)

Kuna kitu inaitwa toxicology. Inawezekana mbuzi mliyekula alikuwa amekula jani lenye sumu fulani kabla hajachinjwa, na hiyo ikawapa reaction kidogo. Jaribu kula tena mbuzi in the same venue uone reaction yake.

(Au kwa sababu hukum'bebea memsahib nae kidogo akakulaani, hehehe)
 
Mmekula Mbwa, sio Makanyaga bar Moshi?

Jamani yamenikuta hiyo juzi! Nilikula nyama ya mbuzi kwenye bar moja hivi mimi na rafiki yangu.. Baada kama ya nusu saa hivi nikaanza kuwashwa mwilini sana... Mpaka leo ndio imepungua... Nikamuuliza rafiki yangu nae kasema aliwashwa kama mimi...! Hii inaweza kuwa imesababishwa na nini?
 
Huwa una kawaida ya kula mbuzi? Inawezekana ukawa na allergy tu. Pia inawezekana kuwa mafuta yaliyopikia yakawa na reaction kwako (japo sidhani kama ni coincidence kwenu wote wawili itokee)

Kuna kitu inaitwa toxicology. Inawezekana mbuzi mliyekula alikuwa amekula jani lenye sumu fulani kabla hajachinjwa, na hiyo ikawapa reaction kidogo. Jaribu kula tena mbuzi in the same venue uone reaction yake.

(Au kwa sababu hukum'bebea memsahib nae kidogo akakulaani, hehehe)
mkuu Kibada hapa kwenye red nahisi ndio tatizo
 
Last edited by a moderator:
Nilipoona hii comment kwanza nikaingia mtini... Nilitapika usiku nilikuwa nafikiria labda nilikula nyama ya MBWA... Nilienda kwa daktari nilapewa vidonge vinaitwa celestimine kama sikosei.. Nilikunywa kimoja tuu kuwashwa kukapungua... Nimepona sasa lakini bado nina makovu ya kujikuna..

pole sana mkuu, unajua siku hizi hawa wafanyabiashara siyo waaminifu kabisa,ndo maana watu wanafikiria vitu vingi kutokana na matukio ya nyuma.
 
Back
Top Bottom