HII INAFAA KUWEKEA MKAZO (REPOST)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
picha nzuri.jpg


BUSARA KWA WANAWAKE. YAFUATE HAYA MAHUSIANO YAKO YADUMU.


1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima na uthubutu wako.

2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.

3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.

4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.

5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.

6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongera na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.

7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!

8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.

9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.

10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.

11. Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.

12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.

13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!

MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE.
 
Maneno kuntu mkuu,mantiki yake mwanamke mwenye busara, heshima, utiifu, upendo na hekima ni misingi mizuri ya kusimamia na kuishi kwenye kanuni tajwa hapo juu.... Ndoa ama mahusiano yako yatakuwa imara na yenye furaha daima bila ata kumtegemea mganga..
 
Bonge moja la ujumbe na maneno ya maana. Ila sasa, kuna wale 'shupaza shingo', ngoja kwanza waamke utawasikia.
 
Hiviii, kwanini wanaume hawafundishwi haya wakati ndo wa kwanza kuboronga kwenye ndoa? Kila siku wanawake tuuu wakati wanaoharibu wanaachwa waendelee kuharibu.
 
Kwahiyo namsamehe in advance kabla hata hajatenda kosa mmmhhh jaman tuwe wakweli. Mambo mengine hayana maana yaan mwanamke aumizwe tu kisa aki react atakuwa hana hekina na sijui busara eti atakuwa si mke mwema haki ya nani mtuache mkitaka amani basi tushirikiane kujenga mahusiano mema...this is two way traffic
 
Ningekuwa mwanaume ningenenepa hadi sharubu
Make maisha yangu yanguekua kama malkia wa nyuki
Umeshaanza kujifananisha na wanaume thats wrong interpretation sio kumpa heshima mwanaume ni kosa ama ndo anakuwa kama malkia wa nyuki........ Awoman should be submissive to her husband nothing else
 
Umeshaanza kujifananisha na wanaume thats wrong interpretation sio kumpa heshima mwanaume ni kosa ama ndo anakuwa kama malkia wa nyuki........ Awoman should be submissive to her husband nothing else
Naishi maisha halisi maigizo ili kufurahisha watu siwezi...... Siwezi namaanisha siwezi mie ni binadamu nna moyo that's a all
Nikupe mfano tu mwanamke na mwanaume wakifumaniana unahisi nani atalianzisha? Nani ataona katendewa dhambi, kaonewa kadhalilishwa?
Kwanini upande mmoja uhisi hivo ilhali wote mmetenda sawa??? usinipe jibu rahisi kuwa ilikuwepo tangu enzi
 
Back
Top Bottom