Hii ina maana gani wakuu?

Hii ina maana gani wakuu?

Mudi Salah

Member
Joined
Jul 5, 2022
Posts
57
Reaction score
55
Binafsi nilipokuwa miaka 10 nilikuwa na wenzangu tunacheza mpira wa makaratasi na washkaji, pembeni ya ule uwanja kulikuwa na mwembe wenye matunda machache tu basi kuna jamaa alikwea juu ya ule mti akaanza kuzitikisa ili zianguke.

Tulipoona vile wote tukaenda kuaokota kisha tugawane na aliyekuwa amekwea, kwenye mgao mimi nilipata embe 1 nikiwa nakula lile embe kwa muda mpaka kongwa likawa jeupe likatokea embe kubwa na lililoiva vizuri kutoka juu ya ule mti na kutua juu ya kiganja changu na lile kongwa lililoisha utamu likaanguka chini aliyeona hii ni mmoja tu. Kila tukionana hivi sasa huwa ananikumbusha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom