Hii imetokea tandale uzuri

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Niliwahi kumtembelea rafiki yangu mmoja aliyekuwa akiishi na wazazi wake maeneo ya Tandale Uzuri,
Nakumbuka ilikuwa ni majira ya asubuhi hivi, basi nilipokaribia nyumbani kwao, nikakuta kiwingu cha watu halafu kulikuwa na wanawake wawili wadada hivi walikuwa wakizodoana na kutukanana hadharani, na mimi nikaona nisipitwe na udaku wa kitaani, nikajisogeza ili kujua kulikoni.
Walikuwa wakitukanana matusi ya mwilini yasiyofaa kuweka humu, si unajua vituko vya uswahilini?

Basi mara akaja baba mmoja ambaye nilikuja kujua baadae kuwa alikuwa ni mjumbe wa shina katika eneo lile,
Baada ya kuwatuliza ili wapunguze munkari wote walitulia ndipo, yule mama ambaye alionekana kuchonga sana alipoanza kujieleza kwa mjumbe.
Kumbe kisa cha kutukanana kiasi kile ni mavi ya mtoto, mnashangaa nini? Ndio walikuwa wakigombea mavi!
Ilikuwaje, subiri basi niwasimulie, mbona mna haraka nyie?
Haya sikiliza kwa makini.

Ilikuwa ni hivi, huyo dada wa nyumba ya jirani alikuwa akikatiza kwa huyo jirani yake, akamkuta mtoto wa jirani yake amejisaidia haja kubwa uchochoroni, basi kwa uungwana wake akazoa yale mavi na kuyatumbukiza ******, kisha akamshika yule mtoto mkono hadi kwa mama yake na kumjulisha kwamba mwanae amejisaidia haja kubwa hivyo amnawishe, hapo ndipo lilipozuka balaa, yule mama alitaka aoneshwe yalipo mavi ya mwanae, yule jirani yake akamwambia kuwa ameshayatupa ******,

He! kusikia hivyo mama wa kizaramo akaja juu anadai mavi ya mwanae na kumtuhumu jirani yake kuwa ni mchawi na amechukuwa mavi yam mwanae ili akamloge afe kama alivyo wauwa wanaae wawili.
Kumbe yule mama aliwahi kupoteza wanae wawili waliofariki kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano, hivyo alipoenda kwa mganga akaambiwa kuwa kuna jirani yake ndiye anaemuulia watoto wake.

Bada ya kumegewa mkasa huo na wakuda nikajimuvuzisha kwa rafiki yangu nikawaacha wakiendelea kusuluhishwa na mjumbe wao.

Yaliyojiri huko nyuma yangu siyajui kwa hiyo usiniulize.
 
Hayo ndio matatizo ya maisha ya kuamini au kutegemea ushirikia.Ugomvi kila siku
 
Ni upungufu wa elimu ndio unatupeleka kwenye imani potofu na hili litaondokana palipo na serikali makini yenye kujali wananchi .
 
JAMANI hivi kuna magonjwa mangapi hatari kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano?????

Swali la msingi sana Kiranja..kuna migonjwa kibao yaani mtoto akisalimika after 5yrs toka azaliwe ndo mzee unapumua.Mbaya zaidi mazingira yenyewe hayo Tandale..kule ndo kma uliwakuona ule wimbo wa Suma Lee..uswahili kuna vituko basi tandale ni mojawapo..mtoto anajisaidia hapa mwingine anakandamiza msosi jirani..kunakusalimika hapo??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom