Ndugu zangu hapa mtaani kwetu Kuna mzee mwenye miaka 53 ameoa binti mwenye miaka 25 hii imekuwa tofauti kidogo cos tumezoea Mara nyingi mzee anakuwaga na hela lakini hii couple huyo binti ndio mwenye uwezo wakati mzee hela hana.Huyu binti anafanya kazi bandarini na mzee ni mvuvi wa samaki
Kiukwel binti ni mzuri ile mbaya kuanzia sura paka shape Kuna level tatu hiv
ya uzuri nayo ni beautiful, more beautiful and most beautiful kwangu huyu binti ni most beautiful.couple ya huyu binti na mzee imekuwa ikiibua mijadala hapa mtaani na Kuna wengine walifika mbali nakusema inawezekana huyu binti anajipatia hela kwa njia za kishirikina kwa kupitia kiwa na huyu mzee watu hawataki kukubali hiki kama kinawezekana.
Bahati nzuri mzee wangu(baba yangu) anajua background history ya yule binti cos yeye ndio alikuwa mshenga wa huyo mzee aliyemuoa huyo binti akaniambia kwa kifupi huyo binti baba yake ni mwiingereza na Mama yake ni mtu wa Tabora huyu binti alichukuliwa na baba yake baada ya kumaliza form 4 Tanzania ambapo alipata division 1 baada ya hapo ndo akapelekwa uingereza kusoma lakini pia hata maali ya huyu binti ilikuwa ni mil 3 lakini yule mzee alikuwa na laki 6 ikabidi huyu binti akampa mzee huyo anayependa mil 3 yote ili alipe maali yake Bila hata familia yake kujua cos alikuwa anampenda.
Kitu ambacho nampendea huyu binti Hana maringo ajari kelele za watu blakini pia anashirikiana na majirani kwenye misiba hata mashuuri mbalimbali.Jumamosi ya wiki iliyopita alimfanyia happy birthday huyo mume wake na akaalika baadhi ya majirani wake siku hiyo alimzawadia mume wake ambaye huyo mzee gari aina ya mark x na suti mbili.